Home Habari za michezo WAKATI ISHU YA FEI TOTO NA YANGA IKIWA BADO MBICHI…SHAFIIH DAUDA AMPELEKA...

WAKATI ISHU YA FEI TOTO NA YANGA IKIWA BADO MBICHI…SHAFIIH DAUDA AMPELEKA BACCA AZAM FC…

Habari za Yanga

Baada ya Mlinzi wa Yanga, Ibrahim Hamad “Bacca” kuanza mchezo dhidi ya US Monastir, na kuonesha kiwango safi kisha kuitwa katika Kikosi cha Timu ya Taifa na kuonesha kiwango safi.

Kupitia Ukurasa wake wake wa Instagram, Shaffih Dauda ameandika;

Tangu kuondoka kwa Aggrey Moris, Serge Paschal Wawa,Said Morad na Yakub Mohamed, Azam FC hawajawahi kuwa na mabeki wa kati wenye ubora wa juu ndio maana Edward Manyama anatumika pale kati.

Ukihitaji kushinda vikombe hasa ligi kuu ya NBC pamoja na kufika hatua ya makundi au Robo Fainali katika michuano ya Kimataifa basi unahitaji walinzi wenye ubora wa juu ambao wanaweza kupambana kama Ibrahim Bacca.

Ibrahim Bacca hapati nafasi ya kutosha pale Yanga na hii inaweza kuwa njia bora ya maofisa wa Azam FC kumshawishi na kumsajili ili akasaidie pale nyuma kwa sababu huyu kijana ni hazina ya Taifa anahitaji kupata nafasi ya kucheza mra kwa mara.

Azam FC ni sehemu ambayo itamfanya acheze mara kwa mara na kukikuza kipaji chake. Jambo zuri ni kwamba Azam FC ni nyumbani kwa wachezaji wanaotoka Zanzibar.

SOMA NA HII  IMEFICHUKA!!!....MAYELE KUTWAA KIATU CHA DHAHABU...KOMBE LA SHIRIKISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here