Habari za Yanga
Akizungumzia kikosi, Kaze amesema wachezaji Djigui Diarra na Khalid Aucho wataukosa mchezo huo wakitumikia adhabu ya kadi tatu za njano
MECHI YANGA VS TP MAZEMBE…AZIZ KI,AUCHO NA DIARRA WAPIGWA CHINI
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wamekuwa na muda mzuri wa maandalizi kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa kesho Jumapili
Kaze amebainisha kuwa siku mbili za mazoezi walizopata Lubumbashi zinatosha kuwaweka tayari kwa mchezo huo ambao Yanga inahitaji kushinda
“Tumefanya mazoezi mazuri jana baada ya safari ndefu na pua leo tutapata nafasi ya kujiandaa vizuri na mchezo wa kesho. Wachezaji wote wako vizuri naamini tutakuwa na mchezo kesho,” alisema Kaze.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.