KOCHA YANGA ANATUMIA NDOTO KUPANGA KIKOSI...ALIOTA FARID ANAIFUNGA TP MAZEMBE
Habari za Yanga

KOCHA YANGA ANATUMIA NDOTO KUPANGA KIKOSI…ALIOTA FARID ANAIFUNGA TP MAZEMBE

Marce Ben Komba April 3, 2023 2:43 pm

KOCHA Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameufuatilia mchezo wao dhidi ya TP Mazembe akiwa kwake Ubelgiji wakishinda kwa bao 1-0 lakini akafichua kwamba usiku wa kuamkia jana aliota kuwa mfungaji wa bao hilo ni Farid Mussa.

Yanga imemaliza kibabe mechi za Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiifunga Mazembe kwa mara ya pili na kufikisha jumla ya alama 13 kileleni.

Nabi amesema baada ya kuota ndoto hiyo wakati wa mapumziko alishauriana na wasaidizi wake kumuingiza Farid mwanzo wa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya ambaye alimuona hakuwa katika kiwango bora katika dakika 45 za kwanza.

“Hii ni mara ya pili niliwahi kuota kama hivi kwa Mayele (Fiston) na alifunga ilikuwa msimu uliopita lakini Sasa ni Farid ambaye hata mazoezini kabla ya kuondoka niliona ameongezeka ubora,” amesema Nabi.

“Nawapongeza sana wachezaji wangu na wasaidizi wangu kwa kusimamia malengo ya klabu yetu vizuri, nilitamani sana kushinda mechi hii ni wajibu wetu kuwafanya mashabiki wetu wawe na furaha.”

Yanga Sasa inasubiri droo ya hatua ya robo fainali kujua watakutana na timu ipi kati ya USM Alger, Rivers United au Pyramids.

SIMBA YAKOMBA TUZO HIZI CAF…MAPYA YAIBUKA…ISHU NZIMA IKO HIVI AZAM FC YATOLEWA NJE USAJILI WA MCHEZAJI HUYU…WATEMWA WAO NA 200MIL ZAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply