Hii ni kusema kuwa Simba wameamua kuwatumia salamu za wazi watani zao Yanga na wapinzani wao wengine kwa kimataifa, wakidai mchezo wao na Raja Casablanca wamepata somo la kuwamaliza wapinzani.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa, mchezo wao na Raja ulikuwa ni kipimo tosha cha kuona ni kiasi gani watakwenda kuwavuruga wapinzani kwenye mechi zao ngumu zijazo.
Ally alisema, walichojifunza Morocco ni mbinu za ndani na nje ya uwanja, kwa maana benchi la ufundi limepata mbinu mpya na kwa upande wa mashabiki wamepata somo ambalo linakuja kutumika kwenye mechi zao ili kuwavuruga wapinzani.
“Tulifungwa mabao 3-1 na Raja Casablanca, tunajivunia sana mchezo ule kwa sababu umetufunza mambo mengi na kutupa picha ya kuiendea michezo yetu migumu.
“Benchi la ufundi limeondoka na kitu, mimi nimepata jambo ambalo nakwenda kufanya na mashabiki wangu kwenye kushangilia ili kuwavuruga wapinzi.
“Wote waliona namna ambavyo mashabiki wa Raja walivyokuwa wanachizika. Ile sasa nataka ije Simba, nataka wapinzani wavurugwe,” alisema Ally..