Pamoja na milango kufunguliwa mapema lakini bado idadi ya mashabiki waliofika uwanjani kishuhudia mchezo wa Ihefu na Simba ni ndogo.
‘Tangu saa 5 asubuhi milango ilikuwa wazi kwa kiingilio cha Sh 10, 000 mzunguko kushuhudia mechi hiyo itakayopigwa leo saa 10 jioni.
Licha ya idadi hiyo ndogo, uzi mwekundu ndio unaonekana kwa wingi katika viunga vya Ubaruku ulipo uwanja wa utakaotumika kwa mchezo huo.
Asilimia kubwa waliopo nje ya geti ni wajasiriamali haswa mamantiliye wanaouza chakula na vinywaji ambao wametumia fursa ya mechi hiyo kupata riziki.
Mmoja wa mashabiki wa soka Faustine Kanwa amesema umbali, siku kuu na viingilio inaweza kuwa sababu za idadi kupungua.
“Kwanza watu bajeti imeishia kwenye siku kuu,lakini kiingilio hicho naona ni kikubwa lakini zaidi huku ni mbali”
“Hesabu mtu atoke Dar es Salaam alale aidha Mbeya asubuhi safari ya Mbarali hizo gharama zote ni kubwa, ingekuwa Sokoine angalau ingepunguza” amesema Kanwa.