Habari za Simba
Habari za michezo

ZA NDAANI KABISAAA…HIZI HAPA SABABU ZA MOSES PHIRI KUPOTEANA SIMBA…BALEKE AONGEZA KITU..

admin April 10, 2023 10:24 am

Kuna kipindi cha nyuma niliwahi kuwaambia mashabiki wa Simba sehemu fulani kuwa siku simba ikipata natural no 9(Namba 9 asilia) na akaingia kwenye mfumo vizuri basi Phiri atakaa benchi.

Ilikuwa ngumu kunielewa sababu Phiri alikuwa moto ila ndicho nilichagua kuamini. Kwa nini?

Kinachomfanya Phiri apate tabu kwenye soka letu ni kuwa muda mwingi anacheza kama play maker (mchezeshaji) na si finisher.

Soka letu la Tanzania linahitaji no 9 awe finisher zaidi kuliko kuwa play maker, yaani wewe uwe mkali kwenye kuweka mpira wavuni. Ndio maana Mayele anasemwa mchoyo ila anaufalme wake Yanga sababu anaweka Mpira wavuni.

Baleke anasemwa hana dribbling ability kubwa ila hajali yeye kila akiaminiwa na kocha anaweka Mpira wavuni ndio maana taratibu ameanza kujenga ufalme mpya kabisa pale simba.

Kama Baleke hatachuja basi inaweza kuwa mwisho wa zama nzuri za Moses Phiri pale Simba.

MBRAZIL SIMBA AWATUPA DONGO HILI ZITO YANGA…MAYELE ATUMA SALAMU MSIMBAZI HUYU HAPA MTANZANIA ALIYEPATA SHAVU CHELSEA ….SASA HIVI ANAKIPIGA LIGI YA MCHANGANI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply