Habari za michezo
BAADA YA YANGA KULA KICHAPO…SHABIKI HUYU MWANACHI AFARIKI…ISHU NZIMA IKO HIVI
Marce Ben Komba
April 17, 2023
2:36 pm
Shabiki wa Yanga aitwaye Jane, mkazi wa Kata ya Bwilingu wilayani Chalinze mkoa wa Pwani, amepoteza maisha wakati akiangalia mchezo wa jana wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga.
Imeelezwa kuwa shabiki huyo alipatwa na presha na kuanguka ghafla.
Katika mchezo huo uliopigwa Aprili 16 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ulishuhudia Simba wakimaliza uteja wa miaka mitatu kwa kuitandika Yanga mabao 2-0, ambayo yalipachikwa na Inonga Baka na Kibu Denis.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.