KANOUTE ANASUMBULIWA NA NYYONGA...SIMBA WASHINDWA KUVUMILIA WAFUNGUKA HAYA
Habari za michezo

“KANOUTE ANASUMBULIWA NA NYONGA…SIMBA WASHINDWA KUVUMILIA WAFUNGUKA HAYA

Marce Ben Komba April 18, 2023 2:37 pm

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wameeleza kilichomfanya nyota wao Sadio Kanoute akosekane kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Yanga SC pamoja na mechi nyingine zilizotangulia zikiwemo mbili dhidi ya Ihefu FC.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 18, 2023, Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, alisema, Kanoute alipata majeraha ya nyonga hivyo ataingia kambini leo na kisha kufanyiwa vipimo kujua kama anaweza kuendelea na mazoezi au la.

“Kanoute, anasumbuliwa na nyonga, atakutana na madaktari leo kujiridhisha kama yupo fiti ataanza mazoezi,” alisema Ahmed.

Ahmed alisema, mwingine ambaye alikuwa majeruhi ni golikipa namba moja Aishi Manula ambaye naye leo atawasili kambini na madaktari wataangalia, kama tatizo lake linaweza kupona lenyewe au atahitajika kufanyiwa upasuaji.

Kuhusu Agustine Okrah, Ahmed alisema alishapona siku nyingi, alianza mazoezi lakini hakuwa fiti kuanza dhidi ya Yanga hivyo anaendelea na mazoezi.

ULE MGOLI WA INONGA UMEANDIKA REKODI HII…UMEVUNJA REKODI YA OKWI MANE ATUPIWA VILAGO BAYERN…DUUH!! APIGWA FAINI HII…KISA KITASA ALICHOMPIGA SANE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply