Habari za michezo
YANGA YAIPITA SIMBA KWENYE KLABU ZENYE THAMANI AFRIKA MASHARIKI…AZAM FC BABA LAO…
admin
April 20, 2023
4:28 pm
Wakati mchezo wa Soka Afrika Mashariki ukizidi kushika hatamu na kuwa mchezo namba moja kwa kupendwa zaidi, vivyo hivyo klabu za ukanda huo haswa kwa nchi za Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda vinazidi kupiga hatua kubwa kimaendeleo.
Tovuti mashuhuri duniani la mambo ya thamani na masoko kwenye mchezo wa kandanda, ya ‘Transfer Market Wolrd’ imeorodhesha thamani ya sokoni kwa klabu za nchi hizo huku miamba ya soka kutoka Tanzania, Simba na Yanga zikishika nafasi ya pili na tatu.
Katika orodha hiyo, klabu nyingi za Tanzania zimechomoza kwa kuwa na thamani kubwa zaidi kuliko klabu za Uganda na Kenya.
Kinara wa Thamani kwenye ukanda huu ni Klabu cha Azam FC ambacho inakadiriwa uwekezaji wlaiofanya matokeo wanayoyapa ndio jumuisho kuu la thamani yao.
Hata hivyo, huenda kigezo cha thamani hizi pia kukaangaliwa na gharamza usajili pamoja na matumizi ya uendeshaji kwa klabu hizo.
Ifuatayo ni orodha ya klabu hizo kwa kuanzia chini kwenda juu:-
Vilabu vyenye Thamani zaidi Afrika Mashariki.
10: Gor Mahia (Kenya) – Value, $572,200
09. Tusker Fc (Kenya) – Value $596,000
08: Rayon Sport (Rwanda) – Value, $600,000
07: Singida Big Stars (Tanzania) – Value: $623,000
06: Kagera Sugar ( Tanzania) – Value $635,000
05: Mtibwa Sugar (Tanzania) – Value: $657,000
04: Vipers Fc (Uganda) – Value: $975,000
03: Simba Sc ( Tanzania) – Value: $ 2.93M
02: Yanga Sc ( Tanzania) – Value: 3: 15M
01: Azam Fc ( Tanzania) – Value: $ 6.98M
Source: Transfer Market World.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.