Home Habari za michezo ALLY SALIM AULA SIMBA SC…ASAINI MKATABA MNONO….MSHAHARA KAMA WA FEI TOTO…

ALLY SALIM AULA SIMBA SC…ASAINI MKATABA MNONO….MSHAHARA KAMA WA FEI TOTO…

Habari za Simba SC

KIPA namba tatu wa Simba SC, Ally Salim amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu baada ya kuonyesha kiwango kizuri dhidi ya Yanga, timu yake ikishinda mabao 2-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Na habari mpya ni kwamba hata mechi leo Jumamosi dhidi ya Wydad Casablanca, Salim ana nafasi kubwa ya kusimama langoni kwani Aishi Manula bado hajakaa sawa na Beno Kakolanya ataanzia benchi.

Namna alivyodaka mechi ya watani, Salim aliwapa amani mashabiki wa Simba SC waliokuwa na hofu baada ya kukosekana mlinda mlango namba moja, Manula aliyeumia dhidi ya Ihefu mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Inafahamika kwamba siku moja baada ya Simba SC kuifunga Yanga, ilikaa na kipa huyo ili kumuongezea mkataba ili aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo huku benchi la ufundi likisema ni hazina kubwa na mechi mbili zilizopita zimemuongezea uwezo wa kujiamini maradufu.

Simba inafanya usajili kimyakimya na wamekuwa wagumu kufafanua mkataba huo kama ilivyomsajili kiraka Yahya Mbegu wa Ihefu ambaye inajulikana kila kitu freshi Msimbazi. Awali Simba ilitaka kumtoa kwa mkopo Salim kabla ya kudaka na Yanga ambayo ni kama imemsaidia kuendelea kusalia klabuni hapo hadi 2027 na akivuta mkwanja mnene wa Sh4milioni sawa na kiwango anacholipwa Fei Toto na Yanga SC.

Inafahamika mshahara wake utakuwa Sh.4 milioni ambayo ni nyongeza ya asilimia 50 ya mshahara wa awali.

Chanzo hicho kilisema “Simba ilijilipua kumpa nafasi Salim na Beno Kakolanya kukaa benchi, mashabiki walikuwa wanahitaji furaha ambayo amewapa, hivyo hakuwa na namna nyingine ya kumuonyesha thamani kwamba amefanya kazi kubwa zaidi ya kumhakikishia kuendelea kusalia Simba.”

Hata hivyo,  hakuwa tayari kufafanua chochote.
Kwa msimu huu Salim hadi sasa amedaka mechi mbili dhidi ya Ihefu, Simba ikishinda mabao 2-0 na Yanga, hivyo ana michezo miwili bila kuruhusu bao.

Ukiachana na hilo, inasemekana tayari kocha wa Simba, Roberto Oliveira amependekeza baadhi ya wachezaji wageni ambao anataka wasajiliwe na ambao anataka watemwe kwenye kikosi chake.

SOMA NA HII  MDOGO WA SADIO MANE ATUA MSIMBAZI KURITHI VIATU VYA LUIS MIQUISSONE