Habari za Yanga SC
Habari za michezo

BAADA YA KUONA WANIGERIA WANAVYOWEWESEKA….MANARA AIPELEKA YANGA MBELE KWA MBELE CAF…

admin April 22, 2023 12:39 pm

Mchezaji wa zamani wa Yanga SC Sunday Manara amesema Yanga wana faida kubwa ya kufuzu hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga SC inaanzia ugenini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Rivers United ya Nigeria, mchezo utakaopigwa kesho Jumapili

Manara ambaye ni mchezaji mwenye rekodi kubwa Tanzania amesema wakati walipokuwa wakicheza kimataifa na wakapata fursa ya kuanzia ugenini kwao ilikuwa bahati kwani walikuwa na uhakika wa kufanya vizuri.

Staa huyo wa zamani amezungumza na kusema kuwa Yanga SC wananafasi ya kuona mbinu zote za wapinzani wao kwa sababu kwao watatoa silaha zote kwani hawatakubali kufungwa uwanja wa nyumbani.

“Wataweza kuwamudu wapinzani wao kwani wanapokuja kucheza nao nyumbani tayari watakuwa wameshafahamu udhaifu wao, naona wana nafasi kubwa ya kwenda nusu fainali;

“Kwa Yanga hii wanaweza kufanya vizuri kwani wataweza kuwamaliza wageni wakiwa nyumbani kiurahisi zaidi kwani hawatakuwa na jipya ila kuzuia wasifungwe,”alisema Manara.

Aliendelea kusema Yanga wanatakiwa kufahamu kuwa watakutana na mashambulizi ya hatari ila watakapokuja nyumbani wapinzani wao watazuia ili wasiweze kufungwa.

SALIM NA CHAMA WAPEWA KAZI MAALUM LEO….MBRAZILI AKESHA NA ONYANGO… MBRAZILI;- MECHI NA WYDAD NILISHAIMALIZA TOKA SIKU NAJIUNGA SIMBA SC…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply