Wachezaji wengi wa mpira wa miguu ambao ni maarufu huwa katika hatari ya kukumbwa na matatizo mengi katika maisha. Baadhi ya changamoto zao ni ndoa zao kuvunjika na matokeo yanawaathiri hadi wanafilisika.
Baadhi ya wachezaji kutoka Afrika waliojipata katika changamoto hiyo:
Taribo West
Staa huyu raia wa Nigeria alifilisika baada ya talaka na kwa sasa ameamua kuwa mchungaji kabisa.
Taribo ambaye alioana na Minigeria mwenzake Atinuke Ekundayo kisha baadaye mwana mama huyo alielekea mahakamani kudai talaka.
Baada ya hakimu kupitisha kesi ya Atinuke, West aliyewahi kuzichezea Inter Milan na AC Milan kati ya mwaka 1997 hadi 2000, alimlipa fidia na ndugu akashuka viwango sana kifedha.
Asamoah Gyan
Mashabiki wengi wa soka wanamfahamu gwiji huyu raia wa raia na penalti aliyoipoteza katika robo fainali ya michuano ya Kombe la dunia mwaka 2010 Afrika kusini.
Lakini pia matatizo ya wanandoa yaliwahi kumfika. Mwezi Oktoba mwaka 2018, ripoti kutoka vyombo vya Afrika na Ulaya zilieleza mchezaji wa zamani wa Ghana, Asamoah Gyan amefilisika baada ya kuachana na mkewe Gifty Gyan.
Gyan baadaye alidhibitisha kuwa amebaki na Pauni 600 tu kwenye akaunti yake ya benki.
Hata hivyo, aligutuka kabla ya hali kuwa mbaya zaidi na mali yake yote akaiandika chini ya jina la kakake ikiwemo nyumba, magari na mali nyingine.
Kisa cha kuvunja mbavu katika kesi ya Gifty na Gyan ni kuwa naye Gyan aliomba watoto wafanyiwe vipimo vya DNA ili kubaini kama ni wake au asilipe fidia.
Emmanuel Eboue