KOCHA SINGIDA BS AITELEKEZA TIMU...KUTIMKIA MAREKANI...ISHU NZIMA IKO HII A-Z
Habari za michezo

HANS PLUIJIM AKIRI KUNYIMWA USINGIZI NA YANGA…CHAKULA HAKIPANDI!

Marce Ben Komba April 25, 2023 7:06 pm

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amekiri kuwa ubora wa kikosi cha Yanga unamnyima usingizi kuelekea mechi mbili ambazo wanatarajia kucheza hivi karibuni.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, kocha huyo amesema kuwa kiwango na matokeo inayoyapata timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, inaonesha namna ilivyo bora hivi sasa.

“Hakuna kocha ambaye anapenda kukutana na Yanga katika kipindi hiki kutokana na ubora wao, hii ni timu ambayo imeimarika sana na wamekuwa wakipata ushindi sehemu yoyote, kitu ambacho kinatupasa kuwa makini,” amesema Pluijm.

Singida Big Stars itacheza na Yanga mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Tanzania Bara Mei 4 na siku tatu baadaye itarudi tena uwanjani kucheza na timu hiyo kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), mechi zote zikitarajia kupigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida.

BARCELONA KUMREJESHA MESSI…WAANDAA DONGE HILI NONO…HACHOMOI!!! HII HAPA IMEVUJA…KOCHA SIMBA ATAJA JINA LA WINGA HUYU…KUSAJILIWA MAPEMA TU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply