EE BWANA!! MAYELE AWEKA REKODI HII YA KIBABE...AMEZUNGUMZA HAYA
Habari za michezo

MASTAA WA YANGA HAWAAMBILIKI…MAYELE ACHACHAMAA…HUYO JOB SASA

Marce Ben Komba April 30, 2023 2:39 pm

Mastaa wa Yanga huwaambii kitu kwa sasa zaidi ya kuwaza ni kwa namna gani watafanikiwa kuweka rekodi ya kufuzu kwenda nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kupitia mchezo wao dhidi ya Rivers leo katika Uwanja wa Mkapa.

Kuelekea katika mchezo huo mastaa wa timu hiyo wameapa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ambayo yatawafanya kuweza kuweka historia ya kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho mbele ya wapinzani wao hao kutoka Nigeria.

Yanga wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 waliyoyapataugenini nchini Nigeria katika mchezo wa kwanza, mabao yalifungwa na straika wao, Fiston Mayele.

Akizungumza nasi, Mayele alisema kuwa wao binafasi wanatambua sehemu ya historia ambayo kila Mwanayanga anaitamani kuiona ikitimia kwa kuwafunga Rivers hivyo lazima wahakikishe kuwa wanapata ushindi ili kutimiza ndoto hizo.

“Kila Mwanayanga anatamani kuona kuwa tunafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na kuwa sehemu ya historia kubwa kwa timu hivyo hata wachezaji na sisi tunata kuwa sehemu ya historia hiyo, tutahakikisha tunatimiza hilo kwa kupambana ndani ya uwanja ili tuweze kupata matokeo mazuri na kufuzu hatua ya nusu fainali.”

Naye beki wa kati wa Yanga, Dickson Job alisema: “Kwa pamoja tunautambua umuhimu wa huu mchezo, hivyo akili zetu zote zipo tukiufikiria. Hakuna ambaye anaona kuwa huu mchezo kuwa umeisha hivyo tutapambana kupata ushindi, tunawaomba mashabiki waje kwa wingi ili tuungane kuleta matokeo mazuri.”

MASHUSHUSHU WA YANGA…WAPATA TAARIFA HIZI NYETI ZA RIVERS…KUMBE WANA MBINU HIZI RAIS ATOA TAMKO HILI ZITO YANGA…BENCHI LA UFUNDI LATAJWA…AMEZUNGUMZA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply