Home Habari za michezo HAWA HAPA WACHEZAJI MAJERUHI WA SIMBA NA YANGA WALIOPONA…LIST KAMILI HII HAPA

HAWA HAPA WACHEZAJI MAJERUHI WA SIMBA NA YANGA WALIOPONA…LIST KAMILI HII HAPA

Tetesi za Usajili Bongo

Dar es Salaam. Kupona kwa nyota majeruhi kunazidi kupunguza presha ya makocha wa Simba na Yanga katika maandalizi ya timu zao kwa ajili ya mechi baina yao itakayochezwa Jumapili ijayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Makocha hao Nasreddine Nabi wa Yanga na Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kila mmoja ana uhakika wa kuwa na wigo mpana wa uteuzi wa vikosi vyao katika mechi hiyo ambayo homa yake imeshaanza kupanda licha ya kila moja kuwa na mchezo mmoja wa ligi kabla ya kukutana.

Hofu kubwa ilikuwa kwa Simba kuwakosa mabeki tegemeo, Henock Inonga na Shomari Kapombe walioonekana kupata majeraha katika mechi mbili tofauti za timu hiyo hivi karibuni lakini benchi la ufundi la timu hiyo limethibitisha ni wazima na wako fiti kuikabili Yanga.

Kapombe aliumia katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca, Simba ikicheza ugenini Morocco na kupoteza kwa mabao 3-1, huku Inonga akitolewa baada ya kuumia katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam juzi dhidi ya Ihefu, Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu aliliambia gazeti hili wachezaji hao na wengine waliokuwa majeruhi wamepona na wameshaanza mazoezi.

“Wachezaji wote ni wazima na walipata majeraha ya kawaida tu ambayo hayawezi kuwafanya wakose mechi. Kapombe alishaanza mazoezi lakini hakupangwa dhidi ya Ihefu kwa ajili ya tahadhari tu, pia anaweza kukosa mechi ijayo ila dhidi ya Yanga atacheza,” alisema.

Yanga nao wanaonekana kuwa kamili kwa ajili ya mechi hiyo kutokana na kupona kwa wachezaji wao wote waliokuwa majeruhi.

Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema; “Hali iko sawa kikosini na tuko tayari kukabiliana na ratiba iliyo mbele yetu. Hakuna mchezaji mpya aliyepata majeraha kwa sasa mbali na Abuutwalib Mshery ambaye alifanyiwa upasuaji na ameshapona na ameanza mazoezi ya kurejea,” alisema Harrison.

Mchezaji majeruhi aliyerejea kikosini kwa Yanga ni Bernard Morrison ambaye alikosekana kwa muda wa miezi miwili.

SOMA NA HII  RASMI...MSUVA NA RONADLO KUKIPIGA PAMOJA...ISHU NZIMA IKO HIVI...