Home Habari za michezo YANGA YAPIGA MKWANJA HUU MZITO…SIMBA MATE YAWADONDOKA…ISHU NZIMA HII HAPA

YANGA YAPIGA MKWANJA HUU MZITO…SIMBA MATE YAWADONDOKA…ISHU NZIMA HII HAPA

YANGA YAPIGA MKWANJA HUU MZITO...SIMBA MATE YAWADONDOKA...ISHU NZIMA HII HAPA

HUENDA hujui, ila ukweli ni kwamba hata kabla Ligi Kuu Bara haijafikia tamati, tayari timu za kumaliza kwenye nafasi Nne Bora kwa msimu huu zimeshafahamika baada ya Singida Big Stars na Azam kujihakikishia nafasi za kuuungana na vigogo Yanga na Simba na kuyakomba mapema mamilioni ya fedha za bonasi kutoka wadhamini wa Azam Media.

Ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Singida dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Liti, Singida na ule wa Azam wa kushinda nyumbani kwa mabao 2-1 mbele ya Mtibwa Sugar zimefanya zifikishe pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 12 zilizopo nyuma yao katika msimamo wa ligi hata kama zitashinda michezo yao yote iliyosalia.

Singida imefikisha pointi 51, ikiwa ni moja zaidi na ilizonazo Azam inayoshika nafasi ya nne, huku Yanga ambao ni watetezi wa taji, ikiwa kileleni na alama 65 ilihali Simba ikiwa ni ya pili na pointi 57 na vigogo hivyo vina kiporo cha Kariakoo Derby kitakachopigwa Jumapili ijayo.

Pambano hilo la watani litakuwa la 100 kwa timu hizo tangu Ligi ya Bara ilipoasisiwa mwaka 1965.

Geita Gold iliyopo nafasi ya tano kwa sasa na iliyokuwa ikionekana kama kauzibe kwa Azam na Singida kabla ya mechi zao za wikiendi hii, kwa sasa ina pointi 34 na ikishinda mechi zote tano zilizosalia za ligi hiyo itafikisha 49, ilihali Ihefu yenye 33 ikishinda michezo iliyosalia itafikisha 48.

Kwa mujibu wa viwango vya fedha ambazo klabu zinazoshika nafasi nne za juu kutoka Azam Media, Yanga hadi sasa kwa nafasi yake imejihakikishia Sh 500 Milioni, huku Simba ikiwa na uhakika wa Sh 250 Milioni, huku Singida kwa nafasi hiyo ya tatu imejiweka kwenye nafsi ya kuvuna Sh 225 Milioni na Azam ikifunga Nne Bora (Top 4) kwa Sh 200 milioni.

Fedha inazopewa timu hizo zinazomaliza katika Nne Bora ni mbali na zile inaztolewa na Mdhamini Mkuu wa ligi hiyo Benki ya NBC.

Ukiachana na hilo, vita ya kushuka daraja bado imepamba moto, japo hali ngumu zaidi ipo kwa Polisi Tanzania iliyo na pointi 19 ikishinda mechi nne itafikisha pointi 31 tu inazoweza kuwapeleka hadi nafasi ya tisa ambayo kwa sasa inashikiliwa na Mtibwa Sugar yenye pointi 29 ambayo nayo kama itashinda mechi zane nne itafikisha alama 41.

Timu inayomaliza kwenye nafasi ya tano itavuna Sh 65 Milioni na inayoifuata nyuma yake yaani ya sita itabeba Sh 60 Milioni, wakati ile ya nafasi ya saba itabeba Sh 55 milioni na itakayofunga pazia la Nane Bora, itaambulia Sh 50 Milioni.

Kwa sasa bingwa wa ligi hiyo ni Yanga ambayo usiku wa jana iliichapa na kuing’oa Geita Gold kwenye pambano la robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) lililopigwa Uwanja wa Azam Complex, na sasa imeungana na timu za Simba, Azam na Singida zimeshatangulia nusu fainali mapema.

SOMA NA HII  YANGA SASA WAMETIMIZA MALENGO YAO SASA WATUONYESHE HILI TU