Ikiwa imepita miezi kadhaa toka asajiliwe na kushindwa kuonekana uwanjani hata kwenye mechi za Kirafiki, Beki wa Yanga SC Mamadou Doumbia amepata mtetezi.
Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe, amejitokeza kumtetea beki huyo kwamba hali anayopitia inatokana na kuimarika kwa viwango vya mabeki wengine kwenye timu hiyo.
Kamwe amedai kuwa Mamadou anauwezo mzuri ila ameshindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza kwa kuwa kuna namba kubwa ya watu wenye uwezo.
“Mamadou Doumbia hawezi kuja tu alafu tumtoe Mwamnyeto ake pembeni, performance yake kwenye mazoezi iko fit kabisa, challenge anazopitia Mamadou ni jinsi gani anaingia kwenye Timu kwa maana ya Chemistry yake na wenzake.
“Ukisajiliwa Yanga unakuja kwenye Squad yenye quality kubwa, unatakiwa upambane haraka uzoee mazingira ucheze kwenye kikosi cha kwanza, hauchezi by favor kwamba umetoka wapi.
“Doumbia Moja ya sababu inayomfanya ashindwe kuingia kwenye kikosi cha kwanza sio kuhusu uwezo wala fitness changamoto yake ni maelewano yake na wenzake (Communication) (language),” amesema