Home Habari za michezo KUHUSU WANAOIHUJUMUA SIMBA…MO DEWJI APEWA NJIA YA KUFANYA…BARBARA ATAJWA…

KUHUSU WANAOIHUJUMUA SIMBA…MO DEWJI APEWA NJIA YA KUFANYA…BARBARA ATAJWA…

Habari za Simba

Mchambuzi na mtangazaji wa Clouds Media, Farhan Kihamu ametoa ushauri wa bure kwa Rais wa Heshima wa Simba SC. Mo Dewji kuhusu namna ya kuirudisha timu hiyo kwenye makali yake.

Chini ni sehemu ya ujumbe aliochapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagrama:-

Tajiri Mo, pale pale ulipoanza na uteuzi wa CEO Barbra kutoka Colombia basi ulipaswa kuendelea kushikilia vision ile ya kimapinduzi kwenye soka, Matajiri wenzako wengi sana wamepita hiyo njia wamefanikiwa.

Kabwela Mimi kutoka Morogoro naweza nisiwe na maana sana ila acha nikupe mifano! Wakati Sheikh Mansour achana na Kaka wa Tandale bali Mansour mwenyewe wa Man City alipoinunua timu alianza na ‘Wakongwe’ kisha baadae akaibadili City mazima.

Alijua anahitaji Watu wa mpira ila dunia ya kisasa ilitaka zaidi vision na mission! Akaenda Barcelona akabeba Ferran Soriano na Xhiki Berigistein, City ile pale na ndoo za kutosha! Aliacha kitu mazoea.

TAJIRI MO, hata Roman Abramovich pale Chelsea alianza na hao Watu wa mpira ikawa timu ya kutumia sana ili ipate mafanikio ila baadae akafanya kama wewe! Akamchukua Mtu wake wa karibu Marina na kumpa timu, the rest is history! Kuna usela aliumaliza hasa usajili na sasa chama lilifika pakubwa.

Tajiri sisemi kuwa ukatae Wanao, mimi sijui mlipotoka ila kila kitu na muda wake, mfumo na njaa zake! Marina hakuaminika ila Cobham ilizalisha sana, Chelsea ilifanya sana biashara na taji la Ulaya wakabeba, tazama kuna kitu cha kujifunza.

Tajiri Mo kila siku unalia watu wanakupiga pesa za usajili, lakini mwisho wa siku? Majibu ni mfumo, kama ambavyo Swahiba wako mwingine GSM kutoka Salamander, ameweka Mtu wake pale Rais wa Yanga na kila kitu wapo front wenyewe, hakuna anayetaka utani kwenye biashara yake.

Sijui naeleweka Tajiri? Leo hii unasikia stori za 10% Jangwani? Leo hii unaona aina ya wachezaji na ubora wao? Wameboresha mfumo na kupunguza watu wengi sana, sasa wana sura nyingi za vijana mpya na ndoto mpya, njaa kali ya underground mithili ya Njombe Mji ama Majimaji.

Tajiri sina mengi ila kinachomtesa PSG kuna namna pia kinakutesa, mfumo mfumo mfumo! Sura zile zile kila siku nadhani ipo haja ya njaa kali mpya ikufikishe sehemu kama ambavyo ulianza kwa Barbra, ndio njia ile.

SOMA NA HII  KISA MECHI DHIDI YA AZAM...NABI APINGA MAAMUZI YA MABOSI WA YANGA...WASALIMU AMRI