Home Habari za michezo USHINDI WA YANGA JANA WAITIKISA CAF….WASAUZI WAJIINGIZA MATATIZONI KWA MCHEZO WA PILI…

USHINDI WA YANGA JANA WAITIKISA CAF….WASAUZI WAJIINGIZA MATATIZONI KWA MCHEZO WA PILI…

Habari za Yanga SC

YANGA ikiwa nyumbani jana uwanja wa Benjamin Mkapa imeichapa mabao 2-0 Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la soka Afrika (CAF) na kutanguliza mguu mmoja katika fainali ya michuano hiyo.

Mabao ya kiungo Stephane Aziz Ki, dakika ya 64 na Winga Benard Morrison dakika ya 90+ yametosha kuifanya Yanga kutanguliza mguu fainali kwani inahitaji ushindi au sare katika mechi ya marudino itakayopigwa Afrika Kusini Mei 17 mwaka huu ili kutinga fainali.

Ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa Yanga kufika nusu fainali ya michuano ya CAF, katika mechi ya jana ilionyesha kucheza kwa ubora na mbinu licha ya kwamba kipindi cha kwanza kilimalizika kwa suluhu.

Katika mechi hiyo, wachezaji wanne walionyeshwa kadi za njano, tatu zikienda kwa Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Kharid Aucho wa Yanga huku moja ikienda kwa Letsie Koapeng wa Marumo. Hakuna mchezaji aliyeoneshwa kadi nyekundu.

Yanga ilipiga jumla ya mashuti 20, lakini ysliyolenga lango ni nane huku Marumo ikipiga nane na manne pekee kulenga lango.

Marumo ilicheza madhambi mara 12 huku Yanga ikifanya hivyo mara 19, pia Yaga iliotea mara mbili na Marumo kuotea mara nne.

Zilipigwa jumla ya kona nane, kila timu ikipiga nne na mechi kumalizika kwa wenyeji Yanga kushinda 2-0.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIZIDI KUCHANJA MBUGA KIMATAIFA...KOCHA YANGA ASHINDWA KUJIZUIA...ATOA DUKUDUKU LAKE...