Tetesi za Usajili
Azam FC

KUHUSU KUMSHAWISHI FEI TOTO….’BOSI KAZI’ WA AZAM FC AVUNJA UKIMYA…AANIKA DILI LILIVYO..

admin May 12, 2023 6:49 pm

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdulkarim Nurdin Amin ‘Popat’ ameshauri kumalizwa kwa hali ya usalama na Amani sakata la Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye amedhamiria kuvunja mkataba na Klabu ya Young Africans.

Kiungo huyo amekwama katika mpango huo kwa zaidi ya mara moja mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ambapo mara ya mwisho alitakiwa kukaa chini na Uongozi wa Young Africans ili kumaliza sakata hilo.

Akizungumza na TBC FM Popat amesema sakata la Kiungo huyo limefikia hatua linaonekana kama kuna uadui kati yake na Uongozi wa Young Africans, halia mbayo sio nzuri kwa ustawi wa Soka la Tanzania.

“Azam FC ni miongoni mwa klabu zilizosajili Wachezaji wengi msimu huu, na Wachezaji wengi wameonesha kiwango kizuri hivyo hatutasajili sana msimu ujao”

“Tutasajili Wachezaji watatu tu na tayari tumeshasajili Wachezaji wawili. Tulimruhusu Sure boy aondoke akiwa kabakiza miezi 8, tulimruhusu Gadiel Michael akiwa bado na Mkataba, mpira sio Uadui.

“Inasemekana nyie ndio mliomshawishi Feisal aigomee Yanga” – Steven Mumbi Mtangazaji.

“Sisi hatuwezi kufanya kitu kama hicho,” amesema Popat.

KIPIGO TOKA AZAM CHAZIDI KUMVURUGA MBRAZILI….AWAPIGIA MAGOTI MABOSI, MASHABIKI… KUHUSU ULE MPANGO WA YANGA KUJITANGAZI UBINGWA…DODOMA JIJI WAIKATALIA YANGA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply