Habari za Simba SC
Habari za michezo

WAKATI RUVU WAKIOMBA MUNGU SAYIWAKUTE LEO…MBRAZILI SIMBA APANGA KUSHINDILIA NONDO…

admin May 12, 2023 10:39 am

Inaweza kuwa ni taarifa Chungu kwa maafande wa Ruvu shooting baada ya kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘ Roberthno’ kusema kwamba wanataka kushinda mchezo utakopigwa leo Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Ruvu shooting.

Robertnho amesema haijalishi kuwa watavuna nini mwisho wa msimu lakini wanachotaka ni kuilinda heshima ya timu.

“Sio mchezo mrahisi kwetu lakini ni lazima tushinde, nimewaambia wachezaji wangu kuwa tunapaswa kumaliza vizuri msimu na mashabiki zetu.”amesema Robertnho

Kocha msaidizi wa Ruvu shooting, Frenk Msise amesema bado hawajakata tamaa wanaamini inawezekana wao kusalia kwenye ligi kwa msimu ujao.

“Kwa uzoefu tulionao tunaamini kwenye michezo mitatu iliyosalia tunaweza kupata matokeo na kusalia kwenye ligi kwa msimu ujao, simba wametuzidi katika uwekezaji ila hakuna aliyejua kama Simba atamfunga Wydad kwahiyo hata sisi tunaamini tunaweza kushinda” amesema Msise

Mpaka sasa Ruvu shooting inaburuza mkia katika ligi hiyo ikiwa na alama 20 hivyo hesabu zao ni kushinda dhidi ya Simba ili kujinusuru na jinamizi la kushuka daraja.

UNAWAZA UTAPATA WAPI PESA ZA HARAKA?…JIBU NI CASINO YA CIRCUS FEVER YA MERIDIANBET…CHEZA SASA.. KUHUS BACCA KUTAKIWA MSIMBAZI…YANGA WAIZIMA SIMBA TENA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply