Habari za Yanga SC
Habari za michezo

KUHUS BACCA KUTAKIWA MSIMBAZI…YANGA WAIZIMA SIMBA TENA….ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin May 12, 2023 10:50 am

Za ndani kabisa zinaeleza kuwa, tayari Klabu ya Yanga Sc imefika makubaliano na Ibrahim Bacca kuongeza mkataba wa miaka mitatu zaidi kuendelea kusalia Jangwani.

Ibrahim Bacca amekuwa na kiwango Bora sana tangu alipoaminiwa katika kikosi cha kwanza Cha Yanga Sc mpaka kuitwa kwa mara ya kwanza timu ya Taifa ya Tanzania.

Baada ya Yanga kutinga nusu fainali ya Kombe lka Shirikisho Afrika, Rais wa yanga, Eng. Hersi Said alisema kuwa wameanza mazungumzo na Bacca ili kuboresha maslahi yake na kumuongezea mkataba kuendelea kuwatumikia Wananchi kwa miaka mingine ijayo.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na mchezaji huyo, zinadai kuwa Yanga wameamua kumuongea mkataba ili kuzuia mianya inayoweza kumfanya akatimka kikosini hapo kutokana na maslahi.

Inataarifiwa kuwa Yanga wamemuongezea mkataba huo ambao pia umeboresha maslahi yake ambapo sasa inasemekana atakuwa akilipwa milioni 6 kwa mwezi.

‘Bacca’ amekuwa sehemu ya wachezaji tegemeo kwa sasa kwenye kikosi cha Yanga, ambapo rekodi za kufurahisha ni kuwa kwenye mechi zote alizocheza, Yanga hawakuruhusu goli hata moja.

Bacca ni miongoni mwa wachezaji wapya waliojiunga na Yanga mara baada ya michuano ya kombe la mapinduzi, ambapo toka wakati huo uwezo wake umekuwa ukiimarika siku hadi siku.

Kwa mabosi Yanga kumboreshea huko mkataba ni wazi sasa jitihada za Simba na Azam zilizokuwa zinamzongeazongea sasa zimekufa rasmi na beki huyo atasalia Yanga labda anunuliwe kwa dau nono.

WAKATI RUVU WAKIOMBA MUNGU SAYIWAKUTE LEO…MBRAZILI SIMBA APANGA KUSHINDILIA NONDO… MBRAZILI AVUNJA UKIMYA SIMBA….ADAI TIMU HAINA WACHEZAJI WAKUPAMBANA…AFUNGUKA MAKUBWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply