Wakati ubishani ukiwa ni mkubwa mtaani baona ya vilabu vya Simba na Yanga juu ya nan kuwa Timu ya kwanza kufika hatua ya Fainali ya Michuano ya CAF.
Rais wa Klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amemaliza utata huku akifafanua kwa undani sababu za Yanga kuwa Klabu ya kwanza nchini.
Akizingumza kupitia kipindi cha Sports Extra, Injinia Hersi amesema;
“Niweke sawa kulikuwa na kombe linaitwa CAF CuP kombe hilo ndio wenzetu walifika Fainali , kulikuwa na shindano lingine linaitwa CAF Winners Cup (Kombe la Washindi) mashindano haya yaliunganishwa mwaka 2004 yakatengeneza CAF Confederation Cup hili ni kombe kubwa liliounganisha mashindano mawili ( CAF Cup & CAF Winners Cup )
Yanga ndio Klabu ya kwanza kutoka Tanzania kushiriki mashindano haya kwenye ngazi ya Nusu Fainali , lakini Yanga iko mguu mmoja kuelekea Fainali , hajawahi kushiriki yoyote kutoka Tanzania kombe hili hatua ya Nusu fainali .
SOMA NA HII WAKATI MAMBO YALIKUWA MAZURI TU...GHAFLA AZAM FC WAMEIFANYIA UKATILI SIMBA KWA BAJANA...