Habari za Yanga SC
Habari za michezo

MAGAZETI SAUZI YAUZA NA STORI ZA YANGA TU….TIMU WENYEJI WAPEWA ‘ODDS’ NDOGO…

admin May 17, 2023 12:10 pm

Baadhi ya magazeti ya hapa Afrika Kusini kwenye kurasa za michezo yameandika kuhusu Yanga kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC siku chache kabla ya mechi ya marudiano dhidi ya Marumo Gallants hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tofauti ya timu hizi mbili [Yanga na Marumo Gallants] ipo hivi, Marumo Gallants inapigana kujinusuru isishuke daraja kwenye Ligi yake wakati Yanga yenyewe tayari bingwa kwenye Ligi ya Tanzania!

Kwa hiyo baadhi ya magazeti yamejaribu kuangalia tofauti ya timu hizi kwa upande wa Ligi zinazoshiriki na umuhimu wa mchezo kati yao.

Yanga ina mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons huku tayari ikiwa bingwa lakini Marumo yenyewe ina mchezo mmoja dhidi ya Swallows wa Ligi ya Afrika Kusini ambao utaamua hatma yao ya kubaki Ligi Kuu au kushuka daraja.

HUU HAPA MKAKATI WA BILIONEA WA YANGA KUHUSU NDOO YA AFRIKA…KAZI INAANZA LEO RASMI… MASHUSHU WA CAF WAVAMIA HOTEL YA YANGA…WATOA ‘DATA’ ZA WASAZUI NA TAHADHARI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply