Levski Sofia dhidi ya AEK Athens Mchezo wa Kufuzu Makundi UEFA Champions League
Mchezo wa leo Jumanne, Agosti 18, 2026, kati ya Levski Sofia na AEK Athens ni mojawapo ya mechi zenye mvuto mkubwa katika hatua ya kufuzu ya UEFA Champions League msimu huu.
Ukichezwa katika uwanja wa Vasil Levski National Stadium, mchezo huu wa kwanza ya raundi ya mwisho ya kufuzu utaamua ni timu gani itakayoingia hatua ya makundi ya kombe kuu la Ulaya jambo ambalo kwa Levski litakuwa mafanikio makubwa ya kihistoria baada ya miaka ishirini ya kusubiri.
Chini ya kocha Julio Velazquez, Levski wamejenga msimu wa ndoto tangu walipovunja ukame wa miaka 17 wa kutwaa ubingwa wa ligi ya Bulgaria msimu uliopita. Safari yao ya kufuzu Ulaya imekuwa ya kuvutia waliwatoa Borac Banja Luka na Universitatea Craiova kabla ya kupambana vikali na Kairat Almaty, ambao waliwafunga kwa jumla ya mabao 2-0 kwa raundi mbili.
Nguvu kubwa ya Levski msimu huu imekuwa ulinzi wao, ambao umebaki imara bila kufungwa katika mechi nne mfululizo, huku wachezaji kama Reinaldo (mabao 5) wakiongoza mashambulizi yao kwa ufanisi.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
AEK Athens, kwa upande wao, wanawasili Sofia wakiwa mabingwa watetezi wa Ugiriki na wakiwa na kambi thabiti chini ya kocha Marko Nikolic. Timu hii imekuwa haijapoteza mechi 13 mfululizo, ikichanganya matokeo mazuri ligini na katika mashindano ya Ulaya.
Hata hivyo, udhaifu wao mdogo umejitokeza kwenye ulinzi, ambako wameshindwa kuwa na “clean sheet” mara nne katika mechi sita za hivi karibuni jambo ambalo Levski wanaweza kulitumia kwa faida yao licha ya kutarajiwa kutumia muda mrefu wakijilinda.
Kimtindo, mechi hii inaonyesha mgongano wa falsafa mbili tofauti Levski wakitegemea nidhamu ya kiulinzi na mashambulizi ya haraka (counter-attack), huku AEK wakipenda kumiliki mpira zaidi na kujenga mashambulizi kwa uvumilivu.
Kwa jumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa wa hesabu na tahadhari kubwa kutoka pande zote mbili, huku kila timu ikijua kosa moja dogo laweza kuathiri ndoto yao ya kufika hatua ya makundi.