Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

MGUNDA APENDEKEZA MBADALA WA MANULA SIMBA…TIMU ‘KIBAO’ ZA SAUZI ZINAMTAKA…

admin May 18, 2023 4:15 pm

Klabu ya soka ya Simba SC imepanga kufanya Maboresho Makubwa katika Timu hiyo na eneo kubwa ambalo watafanya Maboresho kuelekea Msimu Ujao ni eneo la Golikipa, ambapo imeelezwa Kocha msaidizi Wa klabu hiyo Juma Mgunda amependekeza jina la Kipa namba Moja Wa Coastal Union na Timu ya Taifa ya Comoros Mahamoud Mroivili ambaye mkataba wake na Coastal Union unamalizika Mwishoni mwa Msimu Huu.

Tetesi zinasema kwamba kama Simba SC watapata Saini ya Mohamoud atasaini kandarasi ya Miaka Miwili.

Mbali na Simba kuhitaji Saini ya Mohamoud, Timu kadhaa kutoka Nchini Kenya na Afrika kusini zimeonesha nia ya kimhitaji mcomoro huyo.

Mpaka Sasa Mohamoud ana clean sheets 6 kwenye michezo ambayo amekaa langoni akiwa na Coastal Union Msimu Huu.

Timu ambazo amewahi kupita…

Coastal Union FC

Coffee Sport FC ya Ethiopia

Aspl 2000 Club ya Mauritius

Coin-nord Club ya kwao Comoros

Apaches Club ya Comoros

Volcan Club Comoros

Wanamsimbazi vipi Golikipa huyo?

MBRAZILI SIMBA AVUNJA UKIMYA KUHUSU WALIPOFELI MSIMU HUU…ATAJA MASTAA ‘WABOVU’… BAADA YA KUTINGA FAINAL CAF…YANGA WAKATAA ‘VIBE’ LA MASHABIKI DAR….ISHU IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply