Habari za Yanga
Habari za michezo

BAADA YA YANGA KUTINGA FAINAL CAF ….SARPONG ATAMANAI KURUDI KUKIPIGA TENA …

admin May 22, 2023 3:18 pm

Nyota wa Ghana aliyewahi kukipiga katika klabu ya Yanga na Rayon Sports, Michael Sarpong ameeleza kuwa anatamani kurudi Tanzania na kuichezea ligi kuu ya Tanzania kwa mara nyingine.

Sarpong ambaye kwa sasa anaichezea Forest Rangers ya Zambia ameiambia Wasafi Media kuwa hajawahi kuisahau ligi ya Tanzania kutokana na ushindani wake mkubwa uliopo na jinsi inavyozidi kukua na kufanya vizuri kimataifa.

“Napakumbuka sana Tanzania, naipenda ligi Kuu ya Tanzania, inazidi kukua kila siku na inafanya vizuri sana kimataifa, natamani kurejea Tanzania nicheze timu yoyote ambayo naweza kuisaidia ikafanya vizuri zaidi,” amesema Sarpong.

Sarpong alisajiliwa Yanga kwa mbwembwe nyingi ambapo tofauti na matarajio ya watu  alishindwa ‘kupafomu’ na kujikuta akitupiwa lawama .

BAADA YA KUTIKISHWA NA WIMBI LA ‘KUFA KIUME’…MBRAZILI SIMBA AANZA UPYAA…. KUHUSU ISHU YA BALEKE KUSEPA SIMBA…WAKALA WAKE AIBUKA NA HOJA HII NZITO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply