Home Habari za michezo HII HAPA MIEZI MINNE YA MUDATHIR YAHAYA NA MAAJABU YAKE NDANI YA...

HII HAPA MIEZI MINNE YA MUDATHIR YAHAYA NA MAAJABU YAKE NDANI YA YANGA….APEWE MAUA YAKE TU…

Habari za Yanga SC

Wakati akisajiliwa Yanga katika dirisha dogo la usajili lililodumu kwa mwezi mmoja kuanzia Disemba mwaka jana hadi Januari mwaka huu, Mudathir Yahya hakuonekana kama angeweza kupenya ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuachana na Azam FC pindi msimu uliopita ulipomalizika Juni, mwaka jana.

Uwepo wa nyota wa safu ya kiungo ambao walikuwa wanafanya vizuri katika kikosi cha Yanga wakati Mudathir anasajiliwa akina Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki, Yannick Bangala na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ulionekana ungekuwa kikwazo kwa kiungo huyo wa Taifa Stars kupata nafasi kikosi cha kwanza.

Hata hivyo, mambo yamekuwa tofauti na Mudathir ndio ameonekana kujihakikishia nafasi kikosi cha Yanga huku akiwa kipenzi cha kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi.

NGUZO LIGI KUU

Tangu alipojiunga na Yanga hadi sasa, Mudathir amecheza mechi zote kumi za Ligi Kuu ambazo timu hiyo imecheza mara nyingi akiwemo katika kikosi cha kwanza huku mara kadhaa akiingia akiwa anatokea benchi.

Katika mechi hizo kumi, Mudathir ameanza kikosi cha kwanza mara tano na ameingia kutokea benchi mara tano.

Uimara wake katika kuilinda safu ya ulinzi umeifanya Yanga iruhusu mabao sita katika mechi hizo kumi huku ikipata ushindi mara tisa na kupoteza mchezo mmoja tu.

Na Mudathir hajaishia kuilinda safu ya ulinzi tu bali pia ameifungia Yanga mabao mawili ambayo yote yalikuwa ni katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji walioibuka na ushindi wamabao 4-2.

KIMATAIFA HAKAMATIKI

Mudathir amecheza mechi zote kumi za Yanga za Kombe la Shirikisho Afrika kuanzia hatua ya makundi.

Katika mechi hizo kumi, ameanza kikosini mara saba na kuingia kutokea benchi mara tatu huku akicheza kwa dakika 503 katika mechi hizo zote.

Na licha ya kucheza kama kiungo wa ulinzi, aemfunga bao moja katika mechi hizo kumi za Kombe la Shirikisho Afrika.

KIRAKA WA MAANA

Alitegemewa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji lakini Nabi amekuwa akimtumia pia nafasi ya kiungo mshambuliaji na matunda ya uamuzi huo yalionekana katika mchezo wa nyumbani dhidi ya TP Mazembe ambao alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-1.

Kabla ya mchezo dhidi ya Marumo Gallants, Mudathir alikuwa anashhika nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji waliotengeneza nafasi kubwa za hatari akifanya hivyo mara nne.

SOMA NA HII  AZIZI KI ATOA TAMKO HILI KWA MASHABIKI