Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

ANAYEDAIWA KUTAKIWA SIMBA AKOSEKANIKA KWENYE TIMU YAKE….ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin January 5, 2024 4:53 pm

Ili kuhakikisha inaendeleza kiwango chake kwenye Ligi Kuu, Tanzania Prisons imeanza mazoezi huku ikishuhudiwa staa wake Edwin Balua akikosekana huku za ndani zikielezwa tayari amemalizana na Simba SC kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake.

Hata hivyo Balua alivyotafutwa  kueleza sababu za kutoonekana mazoezini amesema bado hajaripoti, huku ishu ya kutua Simba akieleza kuwa ataizungumzia akiwa sehemu nzuri yenye utulivu.

“Mimi bado sijaripoti kambini natarajia wikiendi hii naweza kuungana na wenzangu, naomba hilo nitazungumza nikiwa sehemu nzuri hapa nilipo hapako sawa” amesema staa huyo wa kimataifa wa Tanzania.

Kwa sasa Ligi Kuu imesimama kupisha kalenda ya michuano ya kimataifa na inatarajia kurejea Februari, huku Wajelajela wakishuka uwanjani kuwakabiri Azam FC kwenye uwanja wa Sokoine.

Leo Januari 5, Prisons ikiwa na benchi lake lote la ufundi chini ya kocha mkuu, Ahmad Ally waliendesha program fupi iliyodumu takribani masaa mawili ikiwa ni kuuweka mwili sawa.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Kocha Ally amesema licha ya kwamba wachezaji wote hawajafika lakini kwa asilimia kubwa wamewasili akieleza kuwa wameamua kuanza mapema ili kuendeleza ubora wao.

“Nashukuru vijana wamerejea salama ambao bado ni kutokana na hali ya usafiri ukizingatia safari za mwanzo na mwisho wa mwaka zinakuwa na changamoto zake,” amesema Ally.

Kuhusu usajili kocha huyo aliyeingia kwenye kinyang’anyiro cha kocha bora wa mwezi Desemba amesema bado wapo kwenye mazungumzo ya wachezaji wanaohitajika na hadi Jumatatu wanaweza kuwa wamekamilisha kila kitu.

“Tulipendekeza wachezaji tisa kutolewa kwa mkopo japokuwa inategemeana na timu tunazoomba kuwapeleka zikikubali wapo tutakaoacha pia ili kupisha sura mpya” amesema kocha huyo.

SIMBA WAZIDI KULAMBA MADILI YA UTALII….SAFARI HII NI ZAMU YA ZNZ…. IANZE JANUARI KIBABE KUPITIA SLOT YA SILK ROAD NDANI YA MERIDIANBET CASINO LEO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply