Tetesi za usajili bongo
Habari za michezo

BAADA YA KUWAPOKONYA SIMBA ‘TONGE MDOMONI’ KWA YAHYA MBEGU…SINGIDA WAINGIA ANGA HIZI…

admin May 27, 2023 7:34 am

Klabu ya Singida Big Stars imeendelea kujiimarisha kwenye eneo lake la ulinzi baada ya kudaiwa kukamilisha usajili wa beki wa kulia Nicolas Wadada anayecheza katika kikosi cha Ihefu.

Huu ni usajili wa pili kwa Singida Big Stars baada ya kukamilisha usajili wa Yahya Mbegu ambaye waliipokonya Simba tonge mdomoni.

Habari kutoka Singida zinaeleza kuwa Wadada tayari ameshamalizana na mabosi wa Singida BS na kilichobaki anasubili dirisha la usajili lifunguliwe na atangazwe.

Inadaiwa mabosi wa Singida wanataka eneo la beki ya kulia kuwe na uzoefu kwani tayari ilishamtoa kwa mkopo Juma Abdul kwenda Kitayosce kabaki Paul Godfrey ambaye na yeye hapati nafasi ya kucheza mbele ya Nicolas Gyan.

Kuingia kwa Wadada kutatoa mwanga kwa benchi la ufundi la Singida kwani eneo hilo tayari kutakuwa na wa chezaji wawili ambao wana kiwango kizuri na kikubwa wakiwa wanaenda kimataifa.

Afisa habari wa Singida BS, Hussein Masanza alipoulizwa juu ya usajili wa Wadada amesema kwa kifupi, “Tusubiri hadi Ligi imalizike kila kitu kitakuwa wazi, kwa sasa Wadada ni mchezaji wa Ihefu kwa hiyo siwezi kuzungumzia sana.”

YANGA WATAJA WATAKAO PATA TIKETI ZA BURE MECHI YA FAINAL KESHO…UTARATIBU NI HUU… KUHUSU DILUNGA KUPEWA MKATABA SIMBA….UKWELI WOTE HUU HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply