Home Azam FC KUHUSU MANULA KURUDI AZAM…JAMBO LINAPIKWA KIMYA KIMYA AISEE…

KUHUSU MANULA KURUDI AZAM…JAMBO LINAPIKWA KIMYA KIMYA AISEE…

Habari za Simba leo

Utake usitake, ila fahamu kwamba tayari Kocha mpya wa Azam FC, raia wa Senegal Youssoph Dabo, ameshapewa mafaili ya wachezaji wote waliopendekezwa kujiunga na kikosi hicho msimu ujao na miongoni mwao kuna majina ya Fiston Mayele, Fei Toto na Aishi Manula.

Hivi karibuni kabla ya Azam FC kuanza safari ya kuelekea mjini Mtwara Kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, walimtangaza kocha wao huyo mpya.

Chanzo chetu kutoka Azam kimesema kuwa, kisa cha kumshusha mapema kocha wao Dabo ni kwa sababu walihitaji kumpatia baadhi ya majina ya wachezaji waliopendekezwa na makocha waliokuwa na timu ili awatazame mapema kabla ya kuwasainisha.

“Tayari kocha yupo nchini na ameshapitia baadhi ya majina ya wachezaji waliokuwa watakiwa na benchi lililokuwa na timu hivyo kazi aliyonayo kwa sasa yeye ni kuhakikisha anawatazama wachezaji hao na waliopo kikosini kisha akiridhika tunatia saini nao,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe alisema: “Ni kweli kocha tumemtangaza mapema ili aweze kutazama wachezaji wote wapya na waliopo maana tunahitaji kusajili mchezaji mmoja mmoja kila kila eneo ila tunapoenda kambi ya maandalizi tuwe na nyota wote wapya.”

SOMA NA HII  MANARA AIBUKA NA HAYA MAPYA...AWACHANA SIMBA MAKAVU LIVE...ALIVALIA NJUGA JAMBO HILI