Home Habari za michezo TRY AGAIN;- MANZOKI ALIKUBALI KUJA SIMBA TUKASHINDWANA KWENYE MSHAHARA…

TRY AGAIN;- MANZOKI ALIKUBALI KUJA SIMBA TUKASHINDWANA KWENYE MSHAHARA…

Habari za Simba SC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema, amezungumza na mchezaji Cesar Manzoki na kuna uwezekano akajiunga na Simba siku zijazo.

Try Again aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano na chombo cha habari ambapo alisema, waliwahi kutaka kumsajili kwenye dirisha la usajili lililopita lakini bahati mbaya akapata timu China.

“Alikubali kabisa lakini bahati mbaya au nzuri akatueleza kwamba amepata timu China ambayo iliahidi itamlipa mshahara mkubwa zaidi ya wa kwetu hivyo hatukuwa na jinsi tukamruhusu.

“Juzi tu nimeongeanae, nafikiri mkataba wake ukiisha anaweza kuja kucheza Simba sababu yeye mwenyewe ana mapenzi na klabu yetu,” alisema Try Again.

Try Again alisema timu hiyo ya China ilimpa mshahara wa Dola 60,000 (sawa na sh Mil. 140,400,000 kwa wakati huo).

SOMA NA HII  SIMBA YATAJA MASHINE YAO YA KAZI ITAKAYOWAPA USHINDI MBELE YA AL AHLY