Home Habari za michezo MTIFUANO WA USAJILI SIMBA WAANZA…MABOSI WASHINDWA KUAMUA KATI YA DUCHU AU MWENDA…

MTIFUANO WA USAJILI SIMBA WAANZA…MABOSI WASHINDWA KUAMUA KATI YA DUCHU AU MWENDA…

Habari za Simba SC

Mkataba wa Mlinzi wa kulia wa Simba, Israel Patrick Mwenda ndani ya Simba SC unatamatika Mwishoni mwa Msimu huu.

Mvutano Mkubwa ndani ya Uongozi wa kikosi hicho ni kuwa wapo wanaohitaji aendeelee kusalia kikosini humo na wengine wakisema arejeshwe David Kameta ‘Duchu’ anayekipiga Mtibwa sugar kwa Mkopo.

Mwenda alijiunga na Simba Agosti 2021 akitokea Klabu ya KMC, wakati Duchu alijiunga na miamba hiyo ya Kariakoo akitokea Lipuli iliyokuwa chinia ya Suleiman Matola wakati huo.

Hata hivyo, uimara wa beki mkongwe, Shomari Kapombe umewafanya vijana wote hao kushindwa kufua dafu mbele yake, ambapo mara kadhaa wamejipata wakiwa benchi.

Hivi karibuni kulizuka maneno maneno na ugomvi baina ya Kapombe na Israel Mwenda, ambapo ilisemekana wawili hao wamekuwa wakituhimiana kuchezeana kishirikinina.

Hali ilikuwa mbaya mpaka kufikia Kapombe kujitokeza mbele ya vyombo vya habari na kukiri kuna mambo hayako sawa kwa upande wake ambapo kila akipimwa hospitali aonekani akiwa mgonjwa wala ugonjwa wowote.

Baada ya kauli hiyo, Mwenda naye akaja kujibu mapigo kwa kusema aidha aondoke Simba au mkongwe huyo aondoke ampishe yeye, hali iliyomfanya Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili Robertinho kuingilia kati na kuwapatanisha.

Kwa zaidi ya misimu kadhaa sasa, Simba wameshindwa kupata mbadala mahiri zaidi wa kuweza kumsaidia Kapombe, ambapo wakifanya sajili kadhaa wa kadhaa kama sehemu ya kumpa changamoto beki huyo mkongwe.

SOMA NA HII  TIMU YA TAIFA U-17 YATOA KICHAPO CHA KUFA MTU HUKO....WAJIWEKA 'MBELEMBELE' KUFUZI KOMBE LA DUNIA...