Home Habari za michezo AHMED ALLY :- UKWELI MAMBO NI MAGUMU…. ILA MSIMU UJAO SIMBA HAITAGUSIKA…

AHMED ALLY :- UKWELI MAMBO NI MAGUMU…. ILA MSIMU UJAO SIMBA HAITAGUSIKA…

Habari za Simba SC

Wakiwa kama tayari washahitimisha msimu wa 2022/2023, Klabu ya Simba imesema msimu Ujao utakuwa moto hasa baada ya kujua wapi walipokosea msimu huu.

Simba wapo nyuma ya Yanga kwa alama 7 huku Ligi ikiwa imebaki michezo mitatu kumalizika wana nafasi ndogo sana ya kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu Msimu Huu.

Upande wa Kombe la Azam Sports Federation ndoto zao zilifia mikononi mwa matajiri wa Jiji Azam FC jana Jumapili baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 mchezo wa Nusu Fainali.

Ligi ya Mabingwa tayari walishatolewa na Wydad hivyo ni kama sSimba wataondoka mikono mitupu msimu huu.

Sasa Meneja wa Habari wa Simba Ahmed Ally, akizungumza mara baada ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Azam Sports ambako Simba ilitupwa nje na Azam FC amesema;

“Ni kama msimu wetu kwa mwaka huu umetamatika leo kwa sababu kotekote mambo ni magumu, lakini niseme viongozi wapo na wameona kila hatua tuliyopitia kuanzia Kimataifa mpaka Michuano ya ndani”

“Niwaambie tu tayari mipango ipo tayari na kinachosubiriwa ni Mwalimu tu aseme anamtaka nani na viongozi watamshusha na nitoe angalizo msimu ujao jipangeni, Simba hatugusiki”

SOMA NA HII  ODDS ZA AFCON LEO ZIMEKUJA NA UHAKIKA WA USHINDI WA KIBUNDA...WEKA MKEKA WAKO SASA..