Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MSIMU HUU WAMETOKA KAPA TENA….’TRY AGAIN’ ATAJA SIMBA ILIPOFELI…

BAADA YA KUONA MSIMU HUU WAMETOKA KAPA TENA….’TRY AGAIN’ ATAJA SIMBA ILIPOFELI…

Habari za Simba SC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewaomba radhi Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kwa kushindwa kutwaa taji lolote ikiwa ni msimu wa pili mfululizo.

Try Again aliyasema hayo akieleza kuwa kwenye mpira hali hiyo ni ya kawaida na haipaswi kunyoosheana vidole katika kipindi hiki na badala yake wanapaswa kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Klabu Simba SC ambayo juzi iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambaye bingwa mpya ni Young Africans baada ya kushinda mechi yake dhidi ya Dodoma Jiji iliyopigwa jana Jumamosi (Mei 13).

Baada ya Young Africans kushinda mechi hiyo imefikisha alama 74 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote, huku Simba SC iliyosaliwa na michezo michezo miwili ikiwa alama 67.

Pia, Wekundu hao majuma mawili yaliyopita walitolewa katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa matuta 4-3 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco na baadae kufungwa mabao 2-1 na Azam FC kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ siku tano zilizopita.

Akifafanua kilichowaangusha kukosa makombe hayo, Try Again alisema ni majeraha yaliyokuwa yakiwaandama wachezaji wao, wachezaji wapya waliowasajili walioshindwa kuonesha ubora na ugumu wa mechi za Ligi Kuu.

“Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, nachukua nafasi hii kuwaomba radhi Wanasimba wote, hatukuwa na msimu mzuri sababu tumekosa mataji yote.

Tumekuwa na changamoto ya majeruhi kikosini, wale tuliowaongeza pia wameshindwa kuonesha ubora lakini ndio mpira tunajipanga kwa msimu mpya,” amesema Try Again.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUTEULIWA NDANI YA YANGA....BINKLEB ATOA MASHARTI..AITAJA GSM