Home Habari za michezo PAMOJA NA KUBEBA UBINGWA WA LIGI….INJINIA HERSI BADO ‘AKUNJA USO’ YANGA…TAMKO LAKE...

PAMOJA NA KUBEBA UBINGWA WA LIGI….INJINIA HERSI BADO ‘AKUNJA USO’ YANGA…TAMKO LAKE HILI HAPA..

Habari za Yanga

Baada ya juzi Jumamosi kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ameweka wazi kuwa bado hawajamaliza, msimu sasa mipango yao ni kuhakikisha wanashinda makombe ya michuano miwili iliyosalia ambayo ni Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Yanga juzi Jumamosi wakicheza nyumbani kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara na kutangazwa rasmi kuwa mabingwa baada ya kufikisha pointi 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Mpaka sasa Yanga wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya mashindano mawili ambayo wanashiriki ambayo ni Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la Shirikisho la Azam Sports ambapo kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants utakaopigwa keshokutwa Jumatano nchini Afrika Kusini kikosi cha jana Jumapili alfajiri kiliondoka nchini kupitia Ethiopia.

Akizungumza nasi, Hersi alisema: “Kwanza naweza kusema haikuwa kazi rahisi kwenye safari ya ubingwa msimu huu kutokana na ushindani mkubwa tuliokuwa nao, lakini nawapongeza wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki wetu kwa kuwa kwa umoja wetu tumefanikisha lengo hilo.

“Ni jambo kubwa kushinda ubingwa huu lakini bado tuna kazi kubwa mbele yetu ambayo bado hatujamaliza, tuna nusu fainali mbili za Kombe la Shirikisho Afrika na lile la mashindano ya ndani tunaamini ubingwa huu utatubeba na kutupa ari ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo yaliyosalia.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHINDWA KUWASAJILI AZIZ KI NA ADEBAYOR...AHMED ALLY AIBUKA NA HILI...ADAI HAWAKUWA NA HADHI...