Home Habari za michezo HISTORIA YAANDIKWA….YANGA WAENDELEZA WALIPOISHIA SIMBA…WASAUZI WAPANIKI…

HISTORIA YAANDIKWA….YANGA WAENDELEZA WALIPOISHIA SIMBA…WASAUZI WAPANIKI…

Habari za Yanga SC

HISTORIA Imeandikwa. Ndivyo unaweza kusema baada ya klabu ya Yanga kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza ikiwa ugenini katika Uwanja wa Royal Bafokeng, mjini, Rustenburg nchini Afrika Kusini.

Naam! Yanga imetinga fainali hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kushinda mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali dhidi ya Marumo Gallants kwa mabao 2-0, na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-1, kwani katika mchezo wa kwanza ikishinda 2-0, nyumbani uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na washambuliaji Fiston Mayele dakika ya 45 na Kennedy Musonda aliyetupia dakika ya 61.

Katika nafasi nyingine, Mshambuliaji wa Yanga, Mayele amefikisha mabao sita katika michuano hiyo msimu huu na kuwa sawa na mshambuliaji wa Marumo, Ranga Chivaviro aliyefunga bao moja leo la kufutia machozi.

Mastaa wa Yanga waiocheza mechi ya leo na kuweka historia ya kuhusika moja kwa moja kwenye kuivusha timu kutoka nusu fainali hadi fainali ni Kipa Djigui Diarra.

Mabeki, Dickson Job, Shomari Kibwana, Bakari Mwamnyeto, na Ibrahim Hamad ‘Bacca’.

Viungo ni Yanick Bangala, Kharid Aucho/Stephane Aziz Kii, na Mudathir Yahya huku mawinga wakiwa Tuisila Kisinda/Jesus Moloko, na Farid Mussa.

Washambuliaji waliocheza leo ni Mayele, Kennedy Musonda na Clement Mzize.

Yanga fainali itakutana na mshindi wa jumla kati ya Asec Mimosas ya Ivory na USM Alger ya Algeria.

Ikumbukwe fainali zitachezwa mechi mbili nyumbani na ugenini na Yanga itaanzia nyumbani uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA UGANDA...KOCHA TAIFA STARS ATAMBA KUANDAA 'PILIPILI KICHAA' NYINGI ZA USHINDI....