Home Habari za michezo KISA YANGA KUPONGEZWA NA MO DEWJI….KAMWE AIBUKA NA HILI JIPYA…’AMNYEA’ AHMED ALLY...

KISA YANGA KUPONGEZWA NA MO DEWJI….KAMWE AIBUKA NA HILI JIPYA…’AMNYEA’ AHMED ALLY ..

Habari za Yanga SC

Kutoka kwa Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe amejibu andiko la Afisa Habari wa Simba SC kwamba Yanga ilicheza na timu dhaifu ndio maana imefika Fainali Kombe la Afrika #CAFCC.

“Huyu ni @moodewji.. Nje ya Utani wetu wa Jadi… Huyu ni Mwanadamu aliyewekeza jasho, muda na fedha zake nyingi kwenye Football ya Tanzania

Anajua ugumu wa kucheza Fainali ya CAF .. Na ndio sababu ameipongeza @yangasc kwa Kufikia Mafanikio hayo.. @moodewji Anajua Yanga kucheza Fainali ya CAF ina maana kwa Taifa letu..

Halafu anaibuka kiongozi wa Chini ndani ya Taaisisi inayoongozwa na @moodewji anaweka andiko reeefu lisilo na kichwa wala miguu anabeza … This is Sad.

Iliposemwa ukiwa na Furaha au Huzuni sana Usizungumze au Kuandika Lolote.. Wakubwa walimaanisha mengi sana.

Muda ambao viongozi wao wanatakiwa kuwa watulivu na kufanya Tathmini ya Timu yao, wapi walikosea ili waboreshe wasiwaumize tena Mashabiki wao.

Wao wako busy kufanya tathmini ya Safari ya Mafanikio ya @yangasc Juzi mmoja kajisifia kutimiza Ahadi yake ya kuifunga Yanga Leo mwingine kaja na andiko kuhusu Yanga kwenye Michuano ya Kimataifa

Haya ni mawazo ya watu wadogo kwenye Timu ndogo… KOLO ANAELEKEA HUKO KWA WATU ALIOKUWA NAO”.

SOMA NA HII  BAADA TA KUITUNGUA SIMBA KWA GOLI LA 'KIULAYA ULAYA'....FEI TOTO AFUNGUKA HALI ILIVYOKUWA UWANJANI...