Home Habari za michezo IBRAHIM ‘BACCA’..UNAAMBIWA MPAKA CHIPS KAUZA…AFUNGUKA ‘MASHOGA’ KUMSUMBUA INSTA…
- Habari za michezo
- Habari za Yanga
- Habari za Yanga Leo
- Michezo
- Michezo Bongo
- Michezo Soka la Bongo
- news
- Yanga SC
Kauli za makocha wa Yanga, Nasreddine Nabi na Msaidizi Cedrick Kaze, walipomwambia ni fundi ukifika muda wa kucheza Watanzania wataona kipaji chake, ilimpa moyo wa kuendelea kufanya mazoezi kwa bidii bila kujali atapata nafasi lini.
Baada ya kocha kuanza kumwamini kikosi cha kwanza anakiri bado ushindani ni mkali, unaomfanya asivimbe kichwa badala yake unamtengeneza ubora wa kiwango chake na kutamani kufanya makubwa kila anapopata nafasi ya kucheza.
Anasema kwa mara ya kwanza wakati anatua kambini wachezaji ambao walikuwa wanamsaidia kumwelekeza mazingira ya timu ni Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ walikuwa wanamsisitiza kutunza blandi ya Yanga popote anapokuwepo.
Anasema hana mambo mengi yakumfanya akumbane na matukio nje ya kazi yake, ila changamoto inakuja anapoposti picha zake kwenye mtandao wa kijamii (Instagram), anakutana na ujumbe mbalimbali DM, ambazo zipo pande mbili za mashabiki anazozifurahia na mbaya.