Home Habari za michezo HII HAPA MASHINE YA MAGOLI YA MARUMO ILIYOWAINGIZA VITANI MABOSI WA SIMBA...

HII HAPA MASHINE YA MAGOLI YA MARUMO ILIYOWAINGIZA VITANI MABOSI WA SIMBA NA YANGA…

Tetesi za usajili bongo

Klabu za Simba na Yanga, zimeingia katika vita nzito ya kusaka saini ya straika wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Ranga Chivaviro.

Simba na Yanga zimepanga kuziboresha timu zao katika nafasi mbalimbali ikiwemo ya ushambuliaji ambayo imeonekana tatizo katika pande zote mbili.

Hiyo yote ni katika kuhakikisha wanaiwakilisha vema nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao ambapo timu hizo zitashiriki.

Sio mara ya kwanza kwa Yanga na Simba kukutana katika vita ya usajili ya wachezaji wa kigeni na wazawa wakati dirisha la usajili linapofunguliwa.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Yanga ndiyo wa kwanza kumfuata mshambuliaji huyo, kabla ya Simba kuingilia kati kuulizia uwezekano wa kuinasa saini yake.

Mtoa taarifa huyo alisema, Yanga ndio wenye nafasi kubwa ya kuipata saini ya mshambuliaji huyo ambaye ni tegemeo katika kikosi cha Marumo Gallants ambao jana walicheza dhidi ya Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Yanga tupo katika vita kubwa na Simba ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Marumo Gallants ambaye ni Chivaviro ambaye leo (juzi) benchi la ufundi litamuangalia kwa mara nyingine atakapoichezea timu yake kwenye Uwanja wa Mkapa,” alisema mtoa taarifa huyo.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alizungumzia usajili wa msimu ujao kwa kusema: “Ni lazima tukifanyie maboresho kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao kwa kufuata mahitaji ya kocha wetu Nasreddine Nabi, tupo tayari kutumia gharama yoyote kumpata mchezaji.”

Kwa upande wa Simba, Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally, alisema: “Bodi ya Wakurugenzi ya klabu imepanga kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kufanya tathimini ya kikosi hiki kabla ya kuanza usajili wa msimu ujao ambao ni lazima uwe tishio.”

SOMA NA HII  SIMBA WAIFUATA COASTAL UNION KWA MIKWARA KAMA YOTE...WASEPA MCHANA NA JUA KALI...