Home Habari za michezo MBRAZILI SIMBA AFANYA KWELI….AKABIDHI ‘FAILI’ KWA MABOSI LENYE MASTAA WA KUTIKISA AFRIKA…

MBRAZILI SIMBA AFANYA KWELI….AKABIDHI ‘FAILI’ KWA MABOSI LENYE MASTAA WA KUTIKISA AFRIKA…

Tetesi za Usajili Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ anaendelea na mpango wa kufanikisha usajili wa baadhi ya wachezaji ambao anahisi watamfaa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Simba SC inatajwa kuwa kwenye mchakato wa kufanya maboresho katika kikosi chao, baada ya mambo kuwaendea mrama kwa msimu wa pili mfululizo, na mpango wa usajili uliofanywa mwanzoni mwa msimu huu unalalamikiwa kama sehemu ya kukwamisha mafanikio waliyoyakusudia.

Kocha ‘Robertinho’ anatajwa kuwa na baadhi ya majina ya wachezaji aliodhamiria kuwasajili kwa kushirikiana na Uongozi wa Simba SC, ambao umeahidi kufanya usajili utakaorejesha heshima ya klabu hiyo msimu ujao 2023/24.

Tetesi zilizokuwepo hivi sasa, Simba SC imepanga kusajili wachezaji wanane pekee, kati ya hao wapo wa kigeni na wazawa wenye uwezo na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa.

Baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuhitajika na Simba SC msimu ujao, ambao ni beki wa kati wa Rayon Sports ya Rwanda, Abdul Rwatubyaye na kipa wa Vipers ya Uganda, Alfred Muderekeza.

Wengine ni kiungo mshambuliaji wa RS Berkane ya Morocco, Victorien Adebayor na kiungo wa Geita Gold, Edmund John.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema kocha huyo tayari ana majina hayo ambayo amepanga kuyakabidhi mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Bara kumalizika mapema mwezi Juni.

Ally amesema mara baada ya mchezo wa mwisho wa ligi kuchezwa Juni 9, mwaka huu, haraka Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC watakutana na Kocha Robertinho kwa ajili ya kuyapitia majina hayo.

Ameongeza kuwa, baada ya hapo haraka uongozi utaanza kazi yake ya kukamilisha usajili huo wa wachezaji ambao wamependekezwa kwa ajili ya kusajiliwa.

“Kilichobaki hivi sasa katika usajili wetu mpya ni utekelezaji wa kuwapa mikataba wachezaji wapya tuliokuwa katika mipango ya kuwasajili msimu ujao.

SOMA NA HII  JEMEDARI SAID:- WALIOFANYA USAJILI WA KINA PETER BANDA NA WENZAKE NDIO WALIOPASWA KUFUKUZWA SIMBA...