Home Habari za michezo HAYA SASA YANGA WASHINDWE WENYEWE TU…CAF YAWAPANGIA REFA ‘MSWAHILI’ MECHI YA JUMAPILI..

HAYA SASA YANGA WASHINDWE WENYEWE TU…CAF YAWAPANGIA REFA ‘MSWAHILI’ MECHI YA JUMAPILI..

Habari za Yanga

Refa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean-Jacques Ngmbo Ndala ndiye atakayechezesha Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili wiki hii Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Ngmbo Ndala atasaidiwa na Mkongo mwenzake Olovier Kabene Safar na Zakhele Thusi Granville Siwela wa Afrika Kusini watakaokuwa wanakimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja kulia na kushoto.

Mchezo wa marudiano utafuatia Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litatoa orodha nyingine ya waamuzi.

Kufika hatua hii, Yanga imeitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini, wakati USM Alger imeitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.

SOMA NA HII  AZAM FC TAYARI KWA AJILI YA KUMALIZANA NA WAARABU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here