Home Habari za michezo KUHUSU DILI LA KIBABAGE KUTUA YANGA MSIMU UJAO …ISHU NZIMA KUMBE IKO...

KUHUSU DILI LA KIBABAGE KUTUA YANGA MSIMU UJAO …ISHU NZIMA KUMBE IKO HIVI AISEE…

Tetesi za Usajili Yanga

Yanga tayari imetangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu inayofikia tamati Juni 9 huku ikiwa ndio timu iliyoruhusu mabao machache kama ilivyo kwa Simba zilizofungwa mabao 15, huku Nickson Kibabage akiwa ndiye beki aliyefunga mabao mengi.

Sasa taarifa za ndaani kabisa ni kuwa Kibabage anatajwa tajwa kunukia kwenye usajili mpya wa Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara Yanga SC.

Yanga ambao leo JUmapili wanakipiga kwenye mchezo Mkubwa wa kihistoria kwa nchi na klabu hiyo kwa ujumla, mchezo wa Fainila ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USMA ya Algeria.

Mabosi wa klabu hiyo tayari wameshaanza mawindo ya kujiimarisha huku mkakati wao ukiwa ni kupata kadri iwezekanvyo vipaji wa wachezaji wa kitanzania.

Na katika mkakati huo, tayari mabosi hao wakiongozwa na Rais wake Injini Hersi wameanza kumfukuzia Kibabage ambaye amekuwa na msimu mzuri ndani ya Singida Big Stars.

Kinachongojewa kwa sasa ni kuona kama Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nabi atampitisha na kuwa sehemu ya mastaa wapya wa Yanga kwa msimu ujao, kisha ofa itumwe kwa klabu yek ya Singida.

SOMA NA HII  SKUDU ATIMKA YANGA, UONGOZI WAFUNGUKA.... ISHU IKO HIVI