Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ametupia jiwe kwa watani wao Yanga baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mabingwa USM Alger kwa faida ya goli la ugenini.
โWamejitahidi nini?? Wamekufa kiume gani?! Wamepambana kitu gani?
Yaani kufungwa na timu ambayo inashika nafasi ya 10 kwenye ligi yao ni kujitahidi
Kufungwa na timu ambayo ni ngeni ni kwenye mashidano ya Afrika ni kufa kiume
Hapo wameambulia fedheha tuu, wamecheza na timu wanayolingana nayo hakuna cha kujitahidi,โ ameandika Ally.
Pia ameandika , UTO kakosa kombe tumefurahi na ukweli hatuwezi kujificha tumefurahi sana
Lakini hii sio aina ya furaha tunayoitaka wana Lunyasi
Sisi tunataka furaha yetu ya kutwaa wa Ubingwa wa Afrika
Ni fedheha kubwa sisi kukaa macho usiku kuangalia UTO anacheza fainali
Pamoja na ukweli kwamba njia yao ilikua nyepesi lakini ukweli mwingine ni kwamba wamejua kuitumia iyo njia ya nyepesi
Sisi hua tunapita njia ngumu ni wakati wa kutafuta namna ya kupita kwenye iyo njia ngumu haiwezi kuwa excuse tena eti tumepita njia ngumu
Tumeshamfunga Al Ahly, tushamfunga Wydad nani mwingine mkubwa kabaki jibu ni hakuna kama hakuna kwanini tusichukue huu ubingwa
Imewachukua UTO miaka 30 kufikia rekodi yetu ya kucheza Fainali ya CAF, Sasa tunapaswa kuweka rekodi mpya Afrika
Tunapaswa kuamka ili tuwe wa kwanza kuweka rekodi mpya ambayo UTO atahangaika kuifikia
Kazi kubwa inatakiwa kufanyika ndani na nje ya Uwanja tena ianze sasa
Tunahitaji wachezaji wenye hadhi ya kutupa ubingwa wa Afrika, hadhi ni pamoja na ubora na kujitoa kwa ajili ya timu yetu
Kuwa na kiongozi mpumbavu kama huyu kwenye taasisi kubwa lazime uwe na mashaka na taasisi hiyo.