Home Habari za michezo SUALA LA MANULA ‘KUPIGWA KISU’ AFRIKA KUSINI…MBRAZILI SIMBA ATOA NENO…

SUALA LA MANULA ‘KUPIGWA KISU’ AFRIKA KUSINI…MBRAZILI SIMBA ATOA NENO…

Habari za Simba SC

MASHABIKI wa Simba wameingiwa na ubaridi kutokana na taarifa kwamba kipa namba moja wa timu hiyo, Aishi Manula atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi minne baada ya kwenda Afrika Kusini kwenye matibabu na kufanyiwa upasuaji, lakini kocha mkuu wa kikosi hicho, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewatoa hofu mashabiki hao.

Manula amefanyiwa upasuaji wa nyama za paja baada ya kuumia katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Ihefu uliopigwa Aprili 7, mwaka huu, Uwanja wa Azam Complex.

“Ni pigo kubwa kwetu sisi kama benchi la ufundi lakini na kwa mchezaji mwenyewe, kila mmoja wetu anatambua umuhimu wake kikosini ingawa hakuna namna zaidi ya kumuombea apone haraka,” alisema Robertinho.

Kocha huyo aliongeza kitendo cha kukaa nje kwa muda mrefu kwa nyota huyo ni ishara tosha anahitaji mbadala wake mapema iwezekanavyo ambaye ataendana na kasi ya mashindano mbalimbali.

“Haina maana waliopo hawafai isipokuwa katika kujenga timu imara nahitaji kuona wachezaji bora wawili kwenye kila nafasi, hii itaongeza ushindani pia kutusaidia wakati wa michuano mikubwa.”

Daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo alisema upasuaji huo umekuwa na manufaa makubwa kwa Manula kwani kwa sasa ameruhusiwa kurejea nchini kwa ajili ya mapumziko na mazoezi madogo madogo.

“Wakati anaumia wengi walikuwa wanaongea mambo mengi bila ya kujua ila sasa inaonyesha ni jinsi gani wameguswa na matibabu yake, tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu arejee mapema iwezekanavyo.”

Majeraha hayo yamemfanya kukosa michezo saba mfululizo ya mashindano mbalimbali kwenye kikosi hicho, hivyo kutoa nafasi kwa kipa namba tatu, Ally Salim huku kipa namba mbili Beno Kakolanya akisotea benchi.

SOMA NA HII  MANARA : TUNAWAHESHIMU SIMBA..WANATIMU NZURI NA WACHEZAJI WAZOEFU..LAKINI.....