Habari za Yanga
Habari za michezo

RAIS SAMIA AENDELEA KUIMIMINIA NEEMA YANGA….AHADI NYINGINE MPYA HII HAPA…

admin June 5, 2023 7:10 pm

Rais Samia Suluhu Hassan ameilipia klabu ya Yanga ndege maalumu ya kuwapeleka mkoani Mbeya kucheza michezo yao miwili ya Ligi Kuu Bara kutokana na mwingiliano wa ratiba.

Jana Juni 4, 2023 Rais Samia aliwaalika Yanga chakula cha jioni Ikulu leo Jumatatu ambapo ratiba hiyo iliingiliana na safari ya klabu hiyo kuelekea mkoani Mbeya.

Akizungumza katika radio ya Wasafi jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Juni 5, 2023 Rais wa klabu hiyo, Hersi Said amesema kutokana na mwingiliano huo wa ratiba uliotokea Rais Samia ameilipia Yanga ndege maalumu kuwapeleka Mbeya baada ya chakula cha jioni.

“Ndege yetu ambayo tulitakiwa kuondoka nayo kwenda Mbeya ilikuwa ni saa 1 usiku lakini kwasababu ya mwaliko wa Rais Ikulu leo jioni tulimpa taarifa kuhusu safari yetu na sasa amelipia ndege maalumu kutupeleka Mbeya,”amesema Hersi.

Hersi amesema ndege hiyo iliyolipiwa na Rais Samia itaondoka saa 5 usiku baada ya kumaliza mazungumzo na chakula cha jioni

“Akasema nyinyi vijana wangu njooni kwa ajili ya chakula cha jioni tutazungumza na baada ya hapo sasa ndege maalumu itawapeleka Mbeya,” amesema

Yanga ambaye ni bingwa mara 29 wa Ligi Kuu Bara atakuwa mkoani Mbeya katika mechi dhidi ya Mbeya City itakayopigwa kesho Juni 6, na kumalizia na Tanzania Prisons Juni 9, 2023.

Yanga imepata mwaliko huo na Rais Samia baada ya kumaliza mshindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) mwaka 2022/2023.

AZAM FC WAANZA FUJO ZA USAJILI BONGO….WABEBA KIFAA HIKI CHA AL HILAL YA SUDAN KIBABE… SUALA LA MANULA ‘KUPIGWA KISU’ AFRIKA KUSINI…MBRAZILI SIMBA ATOA NENO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

One response to “RAIS SAMIA AENDELEA KUIMIMINIA NEEMA YANGA….AHADI NYINGINE MPYA HII HAPA…”

  1. Mike Brighton mwanza says:

    Mwandishi usiendelee sana kuna watu wanatafuta sumu iko wapi ili wafe

Leave a Reply