Home Habari za michezo KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA…..NABI ALITAKA KUSEPA NA FEI TOTO DILI LIKATIBUKA...

KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA…..NABI ALITAKA KUSEPA NA FEI TOTO DILI LIKATIBUKA JIONIII…

Habari za Yanga

Kocha Nasredine Nabi ameng’oa nanga Jangwani amegoma kuongezewa mkataba mpya na uongozi ukamtakia kila kheri tayari ameanza mazungumzo na vyuma viwili ambavyo muda wowote watafanya uamuzi wa mwisho.

Baada ya kuapata uhakika anaondoka Kocha Nabi ambaye anahusishwana Kaizer Chief ya Afrika Kusini, aliaaga wachezaji ambao ni mastaa wa timu hiyo walifuchua Kocha huyo alikuwa anaangua kilio mbele yao kabla ya kumaliza kuwaaga.

Inafahamika kuwa Nabi hakutaka kujadiliwa ofa mpya na Yanga kwa vile anankokwenda mshahara wake ni zaidi ya sh70 milioni na atakuwa naposho ya juu. Vilevile alisistiza kwamba anataka Changamoto mpya. Sasa Yanga imetua rasmi kwa hawa wawili ambao mmoja wao atapew mkataba.

FLORENT IBENGE
Ungepiga kura ya mashabiki wa Yanga wangekwambia wanamtaka huyu. Wanamjua vizuri. Mkongomani huyu tayari ameanza kutajwa kuwa ameanza harakati za kuanchana na Al Hilal ya Sudan nikutokana na machafuko ya kisiasa, ni mmoja kati ya makocha ambao ambaye yupo kwenye mazungumzo ya mabosi wa Yanga tangu walipohisi Nabi anaondoka.

Huyu ana heshima kubwa ya kuwahi kutwaa taji la Shirikisho Afrika msimu mmoja nyuma akiwa na RS Berkane.

Ibenge ambaye kwa sasa yuko nchini Morocco akijificha kwa muda baada ya vurugu za kisiasa nchini Sudan, Yanga wanaona haitakuwa vigumu kwake kuja kuendelea na kazi hiyo kutokana na tayari atawakuta wachezaji wengi ambao aliwahi kufanya nao kazi akiwa na timu ya Taifa ya DR Congo ambayo alifanikiwa kuipa nafasi ya tatu kwenye Kombe la Mataifa Afrika pamoja na AS Vita ambaye ameifundisha kwa mafanikio makubwa.

UGUMU ULIPO
Hata hivyo, ugumu pekee kwa Yanga ni kiwango cha fedha ambacho atakihitaji kukubali kusaini mkataba, vyanzo vinaonyesha kuwa akiwa na Al Hilal kwa sasa analipwa dola 50,000, ambazo ni sawa na shilingi milioni 118.8, ingawa Mwanaspoti linafahamu kuwa kocha huyo ni rafiki mkubwa wa rais wa Yanga injinia Hersi Said, tangu akiwa Berkane.

Hivyo inaonekana kuwa anaweza kusaini mkataba ambao unaweza kumruhusu kuondoka muda wowote.

Hersi ana mahusiano makubwa na Ibenge ambapo wawili hao waliwahi kusaidiana kupatikana kwa mastaa wengi wakiwemo Mukoko Tonombe, winga Tuisila Kisinda, Fiston Mayele na hata kiungo mshambuliaji Stephane Aziz KI. Hakuna linashindikana, lakini kama Ibenge atapatikana basi Yanga itakuwa moto zaidi, maagizo yake kukote alipo ni kuhakikisha anakwenda na wasaidizi wake wote.

OMAR NAJHI
Yupo kwenye heasabu za Yanga. Wanamfikiria zaisi huyu. Ni jina kubwa kwenye soka la Morocco lakini anakuja na umaarufu wa kawaida kama ilivyokuwa kwa Nabi. Kocha huyu raia wa Morocco ambaye pia ana uraia wa England, Omar Najhi ambaye amewahi kuifundisha Wydad Athletic ya nchini humo akiwa kama kocha msaidizi naye yupo katika hesabu hizo.

Najhi mwenye leseni ya ukocha ya juu ya Ulaya Pro akiwa na ile ya CAF A, hapa Afrika mbali na kufanya kazi Wydad msimu wa 2021/22, msimu huu alikuwa kocha mkuu wa klabu ya Mouloudia Oujda iliyoshiriki ligi nchini Morocco.

Kiungo huyo mshambuliaji wa zamani Wydad, tayari anafanya mazungumzo pia na mabosi wa Yanga katika kuangalia uwezekano wa kumshusha nchini endapo watakubaliana na uongozi wa klabu hiyo.
Hatua nzuri ni kuwa Najhi anajua kuzungumza lugha ya Kiingereza vizuri, Kifaransa na Kiarabu ambapo atahitaji kuwa na msaidizi anayejua Kiswahili pekee kuendeleza pale alipoishia Nabi.

VIJANA SANA

Sio muumini wa mafaza. Anasoka la kuvutia lakinin anapenda wachezaji Vijana.

Hakuna shaka kuwa Yanga inaweza kumpata kwa kuwa mshahara wake unatajwa ni Dola 25,000 saw na shilingi 59.4 milioni ambazo kwa mafanikio ya Yanga zinazungumzika.

PITSO MOSIMANE
Mitandao yote ya Afrika inamusisha na Kaizer Chief kwa Afrika Kusini. Amevunja mkataba na Al Hilal ya Soudi Arabia baaada ya kushindwa kumlipa. Mashabiki Yanga wanapiga presha aje Jangwani.

Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini ambaye juzi tu ameachana rasmi na klabu yake ya A Hilal ya Saudi Arabia aliyoipandisha ligi kuu.

Mosimane ni rafiki mkubwa wa Hersi na tajiri wao Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ ambapo mwanzoni kabla ya kuanza msimu uliomalizika waliwahi kumleta nchini katika kilele cha Wiki ya Wananchi na inaelezwa aliwashauri baadhi ya vitu kuhusu maendeleo ya timu hiyo.

Huyu anatajwa kuwa kocha mweusi Afrika mwenye mafanikio makubwa zaidi Afrika akiwa ametwaa ubingwa wa Afrika Kusini mara tano na Mamelodi Sundowns, ametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu, moja akiwa na Mamelodi na mara mbili na Al Ahly.

UGUMU
Hata hivyo, kipengele kizito ambacho kinaonekana kuwa kigumu kwa Yanga ni ni kumudu gharama za malipo za kocha huyo ambaye nchini Saudia alikuwa akipokea kiasi cha dola 100,000 (Sh 238 milioni kwa mwezi), hatua ambayo inaweza kuwa ngumu kumshusha nchini, lakini pia ukiachana na gharama za mshahara, ni kocha mwenye gharama nyingine kubwa zaidi, akiwa anataka kuishi hotelini muda wote, lakini akihitaji pia wachezaji wakubwa kutoka timu kama Al Ahly, Mamelodi, Esperance, Wydad na wengine wengi.

NABI ANAWABEBA
Wakati mabosi wa Yanga wakijifungia kusaka mrithi wa Nabi lakini kocha huyo anaweza kuleta ugumu zaidi kwa Yanga kutokana na wasaidizi wake watatu kujipanga kutimka naye atakapohamia.

Kuna uwezekano mkubwa akaelekea nchini Afrika Kusini kufanya kazi na Kaizer Chiefs ya huko ambapo mpaka sasa hesabu zinaonyesha mtu wa kwanza atakayeondoka naye ni kocha wa mazoezi ya viungo Helmy Gueldich.

Kocha huyo anamuamini Helmy ambaye alifanya kazi bora katika miaka yao miwili wakiwa na Yanga ambapo aliwapa ubora mkubwa wachezaji kupitia mazoezi yake makali.

Mwingine ni msaidizi wake wa kwanza Cedric Kaze ambaye anafikiria kusepa naye kwenda kuendelea naye, Nabi hajui vizuri sana Kiingereza hesabu zake kama atamchukua Mrundi huyo atakuwa kiunganishi kizuri kati yake na wachezaji watakaowakuta ambao wengi wanatumia lugha hiyo ingawa wao wanaweza kuzungumza Kifaransa na kuelewana.

Kaze kutua na Nabi Chiefs itakuwa ni kama njia ya kumrudisha mshambuliaji Mrundi Bigirimana Caleb ambaye Wasauzi hao walimchukua akitokea Ulaya ambapo kocha huyo anamjua vizuri.
Mtu mwingine ni Khalil Ben Youssef ambaye ni kocha na mtaalam wa kuchambua mechi za wapinzani kupitia mikanda ya video akiwa na miezi michache tu tangu atue klabuni hapo kuungana na Nabi akitokea Tunisia.

Nabi amewapa sharti Chiefs akitaka kutua klabuni kwao na msafara wake wasaidizi hao ili kumsaidia kwa urahisi hatua ambayo bado Wasauzi hao wanakuna vichwa kuangalia jinsi kukubaliana na sharti hilo.

Hata hivyo, hawa wote wanaweza kuondoka kwa kuwa mikataba yao na Yanga imemalizika na hawana uhakika na maisha yajayo kwa kuwa hawafahamu kocha anayekuja anakuja na nani.

KINA DIARRA ITAKUWAJE
Presha kubwa nyingine kwa mashabiki wa Yanga ni kama Nabi ataondoka na mastaa wake wa kikosi cha kwanza lakini eneo hilo bado litakuwa gumu kutokana na sababu mbalimbali.

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra ni mmoja ya watu ambao wanawaweka mashabiki wa timu hiyo roho juu kuhusu mustakabali wake lakini kuna ugumu kwa Wasauzi hao kufanikiwa hilo hata kama Nabi atampendekeza kutokana na kipa huyo raia wa Mali bado ana mkataba wa miaka miwili na Yanga ambao utaanza kuhesabika msimu ujao.

Yanga haitaweza kukubali kirahisi uhamisho huo kwani utawarudisha nyuma zaidi kuanza upya kujenga kikosi hicho kutokana na kipa huyo bora wa msimu wa pili mfululizo kuwa ndio nguzo yao ya mafanikio wakichukua mataji 6 na kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Jambo pekee ambalo linaweza kumfanya kipa huyo akaondoka ni kama Yanga wataletewa ofa kubwa ambayo inaweza kuwashawishi wakamuuza.

FISTON MAYELE
Staa mwingine ambaye mashabiki wa Yanga wanahema ni mshambuliaji wao na mchezaji bora wa ligi msimu uliomalizika Fiston Mayele ambaye endapo Wasauzi hao watasukuma kumtaka anaweza kushawishika.

Mayele bado amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Yanga hatua ambayo itawalazimisha Wasauzi hao kuwafuata mezani Yanga ili wamnunue na uhamisho huo utawataka kutumia fedha nyingi kutokana na ubora mkubwa aliouonyesha mfungaji bora huyo wa Afrika kwenye Kombe la Shirikisho.

Hata hivyo, Yanga inaweza kushusha pumzi endapo Chiefs itamalizana na mshambuliaji Ranga Chivaviro ambaye wako kwenye mazungumzo naye akitokea Marumo Gallants ambapo pia inaweza kuwa nafuu kubwa kwa Nabi ambaye alimpendekeza na kufanya naye mazungumzo mshambuliaji huyo ili aje atue Yanga kabla ya kufanya maamuzi ya kutaka kuondoka.

Endapo Chiefs itamalizana na Chivaviro wakiwa pia na Caleb wanaweza kuwa na safu bora ya ushambuliaji hatua ambayo itawaondoa kwenye mpango wa kutumia gharama kubwa kumchukua Mayele, lakini pia Yanga hawatakuwa na shida kama akiondoka kwa kuwa wapo kwenye mkakati wa kumsajili mshambuliaji wa Al Hilal, Makabi Lilepo.

KHALID AUCHO
Kiungo wa kazi Khalid Aucho naye anaweza kuwa kwenye presha ya kubaki au kuondoka ingawa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Yanga ambapo Nabi anakubali uwezo wake huku klabu yake hiyo mpya inayomuhitaji wakiwa na uhitaji wa mtu kama kiungo huyo.

Hata hivyo, bado kocha huyo hajaonyesha hatua ya wazi kama atafikiria kuhama na kiungo huyo ingawa changamoto kubwa itakuwa ni mahitaji ya kikosi hicho anachopiga hesabu ya kwenda kukifanyia kazi.

YANNICK BANGALA
Kiungo mkabaji Yannick Bangala alishatangaza kwamba endapo Nabi akiondoka naye anaweza kuondoka lakini ubora wa Bangala kwa sasa unaweza kuwa hatua ngumu kukubalika kwa Wasauz na hata Nabi mwenyewe hao akiwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga.

TUISILA KISINDA
Huyu haondoki na Nabi lakini anaondoka Yanga kwa kuwa anatajwa Yanga hawana mpango naye tena hivyo atarejea kwenye timu yake ya Berkane.

Bernand Morrison
Ni mchezaji mwingine ambaye anaondoka kwenye kikosi cha Yanga baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo na mabosi hawana mpango naye tena.

FEI TOTO SASA
Staa wa kwanza ambaye angeondoka na Nabi haraka ni kiungo mpya wa Azam, Feisal Salum Fei Toto ambaye hakuna kitu utakachomwambia ubovu wa kiungo kwa Nabi kisha akakuelewa.

Nabi alikuwa na hesabu ndefu na Fei Toto kumtafutia timu ya kuichezea nje ya nchi ambapo  siku chache kabla ya kumalizana na Azam alimsaka kumwambia asifanye maamuzi ya haraka akitaka kumpeleka Chiefs, hatua ambayo sasa itakuwa ngumu kutokana na bado ana mkataba mpya na Azam.

SOMA NA HII  KISA MECHI YA SIMBA vs MTIBWA KUSOGEZWA MBELE....'MCHAMBUZI' ATOKWA NA 'POVU' LA MWAKA...