Home Habari za michezo KUHUSU TETESI ZA KUTUA SIMBA….BANGALA AANIKA MSIMAMO WAKE NA YANGA…NABI ATAJWA…

KUHUSU TETESI ZA KUTUA SIMBA….BANGALA AANIKA MSIMAMO WAKE NA YANGA…NABI ATAJWA…

Habari za Yanga SC

Mchezaji wa klabu ya soka ya Yanga Yannick Litombo Bangala amethibitisha kwamba bado anayo nafasi kubwa ya kuendelea kusalia kwenye kikosi hicho kwa msimu ujao kutokana na kuwa na mkataba na miamba hiyo ya soka hapa nchini.

Mbali na hayo, Bangala amesema kwamba anajisikia fahari kwasababu amekuwa ni mmoja kati ya wachezaji ambao wameweza kuisaidia timu yake kufika hatua ya fainali katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika huku akisisitiza kwamba bado anatamani kuendelea kusalia hapa nchini kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwa nchi ya Tanzania.

Bangala ameyasema hayo alipohojiwa na kituo cha Manara TV alipoulizwa kuhusu kuondoka kwake kwenye timu ya wananchi kama jinsi ambavyo tetesi mbalimbali zimekuwa zikisikika kwamba huenda kiungo huyo akaachana na waajiri wake, timu ya wananchi, Yanga.

Hivi sasa kuna tetesi zinazagaa nchini ambapo inaelezwa kuwa Kiungo huyo mkata umeme yupo mbioni kujiunga na mahasimu wa Yanga klabu ya Simba SC.

Taarifa kutoka moja ya karibu na mchezaji huyo, zinaeleza kuwa Bangala aliwasilisha hoja ya kutaka kuvunja mkataba wake na Yanga kwa kile kilicobainishwa kuwa hakulipwa sehemu ya pes zake za usajili kwa msimu unaoanza mwezi wa nane.

Katika hoja yake kwa Yanga, Bangala alisema kuwa kiasi cha pesa kilichobaki kitumike kuvunja mkataba wake ili akapate changamoto sehemu nyingine.

Baada ya mabosi wa Yanga kushutikia janja yake hiyo ya kutaka kuondoka , wakamletea makubaliano mapya ya kumtaka asijiunge na klabu yoyote ile ya Tanzania  katika dirisha kubwa la usajili linaloanza kesho kutwa.

Itakumbukwa kuwa makubaliano kama hayo, yaliwekwa kwenye sehemu ya makubaliano ya kumuuza Fei Toto kwenda Azam, ambapo mabosi wa Yanga walitaka mchezaji huyo asije akauzwa kwenda klabu nyingine yoyote ya Tanzania nnje ya Yanga.

Baada ya kupewa makuibaliano hayo, Bangala pamoja na wawakilishi wake walihamaki na kukataa mpango huo, ambapo bado haijawekwa wazi msimamo wao utakuwa ni upi kutokana na Sakata hilo.

Aidha, inaelewa kuwa mbali ya Simba na Azam, Kaizer Chiefs ya Afrika kusini nao ni sehemu ya timu ambazo zinahusishwa kumtaka Bangala.

Hii ni kutokana na Nabi ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Yanga kutimkia kwenye klabu hiyo, huku akidaiwa kuwa ni chanzo cha yeye kumpa Bangala akili hiyo ya kutaka kuvunja mkataba wake na Yanga ili iwe rahisi kwake kumsajili .

Bangala alijiunga na Yanga, misimu mitatu iliyopita, ambapo katika msimu wake wa kwanza timu hiyo haikuambulia kitu, huku akiisadia Yanga kushinda ubingwa katika mismu miwili mtawalia.

Mbali na kuisaidia Yanga kutawala soka la Tanzania, Bangala pia amekuwa sehemu ya wachezaji muhimu wa Yanga ambao wameweka historia kwa klabu hiyo kufika hatua ya Fainal ya Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED YAIPIGA MKWARA YANGA