Mkutano Mkuu Yanga
Habari za michezo

MKUTANO MKUU YANGA:- CHALAMILA ASHINDWA KUJIZUIA …AANIKA MAHABA YAKE JAGWANI…

admin June 24, 2023 2:19 pm

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameibua shangwe kwa Wanachama waliohudhuria katika mkutano mkuu wa klabu hiyo unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).

Chalamila ambaye ndiye mgeni rasmi katika mkutano huo alibua shangwe hilo baada ya kukaribishwa na Rais wa Yanga, Injinia, Hersi Said kwa ajili ya kutoa hutuba yake.

Akizungumza katika Mkutano huo, Chalamila amesema kabla ya kuteuliwa kiongozi alikuwa ni shabiki wa Yanga ila tangu awe kiongozi imebidi abalansi mapenzi yake kwa kila mtu.

“Kuna muda unapokuwa kiongozi inabidi ubalansi hisia zako lakini kiuhalisia mimi ni Yanga japo mke wangu yeye ni shabiki wa Simba,” amesema.

Aidha Chalamila alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa hamasa kubwa ambayo amekuwa akiionyesha katika michezo nchini.

Katika mkutano wa leo jumla ya wanachama waliohudhuria ni 531 wanaotoka matawi 203 kutoka sehemu mbalimbali ya mikoa ya Tanzania.

KUTOKA MKUTANO MKUU: YANGA WAVUNA BILIONI 7 …. KIPA MPYA SIMBA HUYU HAPA….JAMAA ANADAKA MPAKA ‘MBU’….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply