Jezi Mpya za Simba Kimataifa
Habari za michezo

JEZI MPYA SIMBA NI KESHO….BEI YATAJWA MAPEMAAA…

admin June 28, 2023 10:59 am

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kujiandaa kikamilifu kununua jezi mpya kwani mzigo unatua nchini kabla ya sikukuu ya Idd, Juni 29, 2023.

Akizungumza kupitia Simba APP, Ahmed amesema anafahamu mashabiki wana shauku kubwa ya kuvaa ‘uzi’ mpya hivyo wasiwe na mashaka kwani unaingia kabla ya sikukuu ya Idd inayotarajiwa kusherehekewa kesho  Aalhamisi.

“Mzigo ni mwingi na wa kutosha. Niwaambie tu mashabiki wajiandae na shilingi elfu thelathini na tano zao, mzigo utakuwa wa kutosha hata kama mtu atataka awe na jezi kumi peke yake,” alisema Ahmed.

Ahmed alisema, baada ya kuingia nchini, taratibu za kuuingiza sokoni zitafanyika na maduka yote yatakuwa na mzigo kwa wakati mmoja.

BAADA YA KUZIPUNA SIMBA NA YANGA….ISHU NA MORRISON NA AZAM FC IKO HIVI… BAADA YA KUTAKATA CHINI YA NABI….’BACCA’ KAANGALIA UPEPO WA MSIMU UJAO YANGA..KISHA AKASEMA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply